Tuesday, October 9, 2012

Kamati ya Nchimbi yakiri Nguvu kubwa kutumika, yasema si chanzo cha kifo cha Mwangosi


Waandishi wa habari wakimsikiliza waziri wa mambo ya ndani Dk Emanuel Nchimbi, wakati kamati aliyoiunda ilipokutana na waandishi wa habari kutoa taarifa juu ya kifo Cha Daudi Mwangosi




Mjumbe wa kamati ya kufuatilia mauaji ya Mwangosi Kamishna wa Polisi Isaya Mngulu, akijitambulisha kwa waandishi wa habari





Makamu mwenyekiti w kamati ya kufuatlia mauaji ya Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi,Theophil Makunga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani



Dk Emanuel Nchimbi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari





Taarifa ya kamati juu ya Mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi, imesema nguvu zilizotumiwa na jeshi la Polisi Mkoani Iringa hazikuwa sababu ya kifo cha Mwandishi huyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Jaji Mstaafu Stephen Ihema, amesema kuwa licha ya nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi,nguvu hizo hazikuwa sababu ya kifo cha mWandishi huyo, huku akieleza kuwa marehemu alikufa baada ya Polisi kuamriwa kurudi katika magari yao kufuatia kufanikiwa kuwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa katika mkutano ambao kamati hiyo haikuweza kubainisha kama ulikuwa ni wa ndani au wa hadhara.

Aidha kamati hiyo imeshauri mikutano  na maandamano ya vyama vya siasa visiendelee baada ya uchaguzi wowote na shughuli za kisiasa zifanywe bungeni hadi uchaguzi utakapofikia

No comments:

Post a Comment