Mifupa ya mtumwa wa kale inayokadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka
1,700 imepatikana katika sehemu ya Kimu eneo la Bweni wilaya ya Pangani
mkoani Tanga ikiwa bado imefungwa na minyororo katika mikono na miguu.
Akizungumza
katika mahojiano na gazeti hili jana, Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Historia na Akiolojia, Elinaza Mjema,
alisema walikuta mifupa hiyo baada ya kuchimba ardhi wakiwa katika
harakati za utafiti wa mambo ya kale.
Alisema
eneo ambalo mifupa hiyo imepatikana ni lile lililokuwa likitumika kwa
ajili ya kuvusha watumwa kwenda zanzibar katika miaka ya 1,700 na
1,800.
“Eneo hili
tulilokuta mifupa hii lilikuwa likitumika kwa ajili ya kuwavusha
watumwa katika miaka hiyo ambayo biashara ya watumwa ilishamiri na huu
ugunduzi tunaweza kusema ni wa kwanza kutokea katika Afrika Mashariki
hivyo tuna kila sababu ya kujivunia,” alisema Mjema.
Alisema
yeye kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka UDSM wanatarajia
kuchukua sampuli ya mifupa hiy0 na minyororo Novemba 17, mwaka huu ili
kubaini umri wa mtumwa huyo, mwaka aliokufa na umri wa chuma
kilichotumika kama minyororo.
Mjema
alisema wanataka kubaini iwapo chuma hicho kilitengenezwa na Waafrika
au Wazungu na kwamba kama ni Waafrika kitakuwa kimetengenezwa zaidi ya
miaka 1,000 iliyopita.
Nao
baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Pangani walisema ugunduzi huo utasaidia
kuitangaza wilaya yao kwani ni kivutio cha pekee cha utalii na kutakuwa
na ongezeko la wageni wa ndani na nje ya nchi watakaoongeza pato la
wilaya.
via NIPASHE
No comments:
Post a Comment