KUHUSU WIZARA YA ELIMU NA UTAMADUNI NA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA
Kwanza kabisa napenda kutoa shukurani zangu kwa Wizara kwa sababu shule zimeongezeka na vijijini na mijini.
Hii imefanya jamii ya Watanzania wengi kwenda shule hata kama hajafanya vizuri kwenye masomo. Huko shuleni watakuwa wamejifunza kuishi na watu na mambo mengi yaliyoko kwenye jamii.
Kusudio langu kubwa katika ujumbe huu ni kuhusu mitihani ya Taifa, hasa ile mitihani ya kidato cha 4 na cha 6.
Hoja yangu ni kuhusu mtu anapoumwa ghafla akalazwa au mwingine akachanganyikiwa na hawezi kabisa kufanya mtihani akashindwa kutokana na hali yanayokuwa nayo kwa wakati ule, mimi kama mwanajamii na mzazi nilikuwa naomba kipengele kinachosema hata kama mwanafunzi anaumwa afanye mtihani naomba kibadilishwe. Iwe, endapo mwanafunzi ameumwa ghafla na Daktari akathibitisha hivyo, naomba asifanye mtihani bali aahirishe aufanye mwaka unaokuja kuliko kufanya wakati yuko kwenye hali mbaya na matokeo yakaja ameshindwa na wakati hajaumwa alikuwa na maendeleo ya kuweza kufanya vizuri alikuwa nao.
Naomba Wizara kushirikiana na Baraza la Mitihani waliangalie hili kwa maana, haiwezekani mtoto amesoma miaka 4 au 6 halafu inapofikia hatua ya kufanya mtihani wa mwisho wa Kitaifa, kwa bahati mbaya akaumwa ghafla, na jinsi karo inavyoumiza katika masomo, anashindwa kufanya mtihani wake.
Sheria inayoelekeza afanye mtihani halafu matokeo yakitoka vibaya arudie kama mtahiniwa wa kujitegemea, naona hilo halimsadii mwanafunzi husika. Tunaomba sheria hii ibadilishwe.
No comments:
Post a Comment