Sunday, February 3, 2013

IRAN YAFANYA SHEREHE YA MAPINDUZI YA 34 PAMOJA NA MAADHIMISHO YA UZAWA WA MTUME MOHAMMAD S.A.W


Maadhimisho ya  Mapinduzi ya 34 ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran yamefanyika leo, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yaliyo ambatana na Sherehe ya Uzawa wa Mtume Mohammad  S. A. W  yamefanyika, huku Mgeni rasmi katika Sherehe hizo akiwa ni Mh Bi Asha Gharib Bilal Mke wa Makamu wa makamu wa  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Gharib Bilal.
Mwenyekiti wa Taifa Jumuiya ya wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA), Bi, Shamim Khan  amesema kuwa,  wana adhimisha siku ya kumkumbuka Mtume  Mohammad  S.A.W  ili kumuenzi  kwa mema aliyowatendea waislamu wote Duniani.
Bi, Shamim Khan amewapongeza  Watu wa Iran kwa Kusherekea miaka 34 ya Mapinduzi ya Iran ambayo pia yanajulikana kama Mapinduzi ya Kiislam au Mapinduzi ya mwaka 1979.


Mgeni  Rasmi akizungumza katika Maadhimisho hayo ambapo amewataka wananwake wa Kiislamu kuwa na umoja na kufanya kazi kwa bidii.


Mkurugenzi wa  Kituo cha Utamaduni wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bw, Morteza  Sabouri, akizungumza katika Mkutano huo ambapo amesema kuwa  kusherekea Mapinduzi ya Iran ina ashiria  kitendo cha Kuondoa  Madarakani, uongozi  wa  Pahlavi chini ya Shah Mohammed Reza Phlavi na Badala yake kuwepo kwa jamuhuri ya kiislamu.

Mama Asha Gharib Bilal akiwa katika Sherehe hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam., Miongoni mwa walio hudhuria kwenye Sherehe hizo ni pamoja na, Mke wa Mufti wa Tanzania Bi, Makaje  Goso Kombora, Morteza Sabouri Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran.

No comments:

Post a Comment