Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la
Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra
Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo
zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa
imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Uokoaji ukiendelea.....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la
tukio baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo
asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia
Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu
waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni
17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Askari Jeshi wakikokota Jenereta
kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha mwanga unapatikana
kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya giza kuingia.
No comments:
Post a Comment