Mtoto Ramadhani akiwa na Mama yake mzazi baada ya kufikishwa kituo cha Polisi Mbagala |
Ramadhani baada ya kupata huduma ya kwanza (PIicha kwa hisani ya Mwalimu mkuu shule ya msingi Nzasa) |
MWANAFUNZI wa darasa la pili Ramadhan Hamza(8) katika shule
ya Msingi Nzasa, iliyopo Mbagala jijini Dar esSalaam, ameshindwa kuhudhuria
masomo darasani kwa muda wa wiki nne sasa kufuatia kuunguzwa mikono na baba
yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Hamza Ismail.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, mwenyekiti wa serikali
ya mtaa wa Mianzini Abdallah Mzee, alisema tukio hilo lililtokea baada ya mwanafunzi huyo
kurudi nyumbani kwa wazaqzi wake ma kuchukua sh. 100 kwa ajili ya kununua
sambusa kufuatia kukosa chakula baada ya kutoka shuleni.
“Tulipomuuliza alituambia ni baba yake ndiye aliyemchonma na
moto baada ya kumfunga na vitambaa mikononi kisha akawasha moto ingawa mwanzoni
mama yake alitaka kumkingia kifua mumewe ili unyam huu usijulikane”alisema
Mzee.
Alisema harakati za mzazi wa kike kuuficha unyama huo
zilifichwa hadi majirani walipogundua na kuchukua hatua za kumfikisha katika
ofisi ya serikali ya mta na baadae Polisi amabapo alikiri unyama huo kufanywa
na mumewe kwa madai kuwa mtoto wao alikuwa na tabia ya udokozi.
Aliongeza baada ya mzazi wa kike wa mwanafunzi huyo
kufikishwa Polisi taarifa zilimfikia baba mzazi wa kiume ambaye aliamua
kutoroka nyumbanio na hajaonekana hadi leo.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nzasa Kahabi
Mabeyo amethibitisha mwanafunzi huyo kushindwa kuhudhuria masomo baada ya
mikono yake yote miwili kuwa na vidonda vinavyomfanya ashindwe kuhudhuria
masomo ya darasani
Jitihada za kumpata kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke David
Misime kwa lengo la kuelezea hatua walizofikia katika kumtafuta mzazi
aliyetenda unyama huo zilishindikana baada ya simu yake kuiota bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment