Kipondo kikiendelea
HALI ya mambo ndani ya jumuiya ya umoja wa vijana wa
CCM(UVCCM)si shwari kufuatia vijana wa jumuiya hiyo kutwangana makonde
hadharani wakati wa kumpokea mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo Sadifa Juma
Khamis.
Sababu ya Ugomvi huo ni miongoni mwa vijana hao wa UVCCM
kupinga kuchaguliwa kwa mwenyekiti huyo kwa kile walichoeleza kutumika kwa
rushwa pamoja na kueleza kuwa mwenyekiti huyo hana sifa ya kuhudumu katika
nafasi hiyo kwa kuwa umri umemtupa mkono.
Dalili za Vurugu hizo zilianza kuonekana mapema jana mchana
kwa makundi ya vijana wa ccm kufika
katika ofisi za umoja huo zilizopo pembezoni mwa barabara ya morogoro eneo la
fire jijini Dar esSalaam, wakiwa na
mabango ya kumlaani Sadifa pamoja na katibu mkuu wa jumuiya hiyo Martin Shigela.
Majira ya saa 11:28 jioni msafara wa Mwenyekiti wa uvccm
uliwasili katika makao makuu ya umoja huo huku kukiwa hakuna viongozi wa
jumuiya zingine za Chama hicho na kupokelewa na watu wachache waliokuwa katika
maeneo hayo wakitumbuizwa na bendi ya muziki ya Vijana Jaz
Baada ya kluwasili mohja kwa moja msafara huo wa mwenyekiti
wa uvccm ulisalimiana na watu waliojipanga mistari kabla ya kuelekea meza kuu
kwa ajili ya taratibu zingine.
Wakati mwenyekiti huo akiwa anataka kukaa walijitokeza
vijana mbali mbali wakiongozwa na mjumbe wa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Dar
esSalaam, Agustino Matefu na kusimama karibu na meza kuu huku wakionyesha
mabango yao.
Kufuatia hali hiyo kundi lingine la vijana wa CCM liliinuka
katika viti na kuwafuata wenzao waliobeba mabango na kuanza kuwashambulia kwa
ngumi na teke hadi kuwavusha upande wa pili wa barabara na kisha baadhi ya
vijana waliobeba mabango wakiwemo wanawake wakikamatwa nakuingizwa katika ofisi
za umoja huo kwa hatua zaidi.
Baaada ya hali hiyo Katibu wa umoja huo Taifa Martin Shigela
aliinuka na kusema vijana hao wametumwa na kwamba wamerithi tabia za baba zao
katika chama pasipo kutaja ni baba wa namna gani.
Alisema uchaguzi wa umoja huo umeisha na kilichobaki ni
wanachama kukijenga chama chao pasipo kuangaliana machoni na kuwekeana visasi.
“Hii tabia ya hawa vijana ni ya kutumwa tena na baba zao wa
Kmabo katika siasa tunajua wapo walioumia katika hali hii kwa kuwa walitumia
gharama kubwa kwa ajili ya kuwania uongozi na kama wameona kuna uonevu wafuate
taratibu”alisema Shigela
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma
Khamis,alikiri kuwepo kwa harakati za chini chini za kumzuia kupata nafasi hiyo
kwa kile alichoeleza kuwa misimamo yake ndani ya Chama inawatisha wengi.
Alisema hatorudi nyuma katika kukijenga Chama na kama kuna
wakorofi hatosita kuwashughulikia na kama kutakuwa na kikwazo kutoka juu yake
atakuwa tayari kuachia nafasi hiyo kwa ajili ya kulinda heshima yake nay a
Chama.
“Mimi ni mwanajeshi by professional nimefanya kazi hiyo
nikiwa Tanga na sehemu nyingine ya nchi hivyo sitoona taabu kumshughulikia mtu
yeyote atakayekuwa kikwazo kwetu na kama yatanishinda kwa sababu zilizo nje ya
uwezo wangu nitaachia nafasi hii mimi si
mroho wa madaraka”alisema Sadifa
|
No comments:
Post a Comment