Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji imeandaa
mpango wa kupata idadi ya Watanzania waishio nje, idadi ya wahamiaji
nchini pamoja na mchango wao katika kuinua uchumi wa nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, alisema jana kuwa
mkakati uliopo sasa ni kujua idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi
wanachangiaje kuongeza uchumi wa chini kwa kuleta fedha za kigeni
nchini.
Alisema kuna Watanzania wengi wanaishi nje ya nchi huku
wakihudumia familia zao nchini kwa kuwatumia fedha za kigeni na mahitaji
mengine kila siku.
“Lazima tujue wahamiaji wanaichangia katika
nchi yetu kwa kiasi gani, kuna mapato mengi yatokanayo na Uhamiaji hivyo
yatupasa kufahamu ni kwa kiasi gani,” alisema Silima.
Alisema,
waandishi wa habari pamoja na wanasiasa wanapaswa kupewa elimu juu ya
masuala ya uhamiaji na uhamaji kwa kuwa wengi wao hawafahamu faida zake.
Naye
Kamishna wa Fedha na Utawala Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja, alisema
wataalam kuna waliokwenda nje ya nchi kujifunza masuala mbalimbali
kuhusu uhamiaji na uhamaji. Aidha, alisema wataalamu wa takwimu
wanafuatilia kujua idadi ya Watanzania walioko nje.
---
via gazeti la NIPASHE
No comments:
Post a Comment