Sunday, November 25, 2012

NCCR MAGEUZI YATOA 5000 KWA WAANDISHI ILI WAKAANDIKE HABARI YA KUPINGA RUSHWA ILIYOPO CCM

h
Kaimu katibu mkuu wa Chama cha NCCR MAGEUZI Bw, Faustine Sungura akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Ofisi hiyo ambapo alikitaka chama cha Mapinduzi kuhakikisha kuwa rushwa inakomeshwa katika chama hicho ndani ya siku saba na sio miezi sita kama alivyo ahidi  Makamu mwenyekiti wa CCM  Philip Mangula.
 Chama cha Siasa cha  NCCR MAGEOUZI kimejikuta kikiwa katika hali ya kutoeleweka baada ya kuilalamikia Rushwa iliyopo katika chama Mwenzake CCM kwa kusema kuwa itawashugulikia viongozi wake walioingia madarakani kwa Rushwa baada ya miezi sita  wakati huohuo NCCR ikatoa Rushwa kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo leo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano huo, Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw, Faustine Sungura, amesema kuwa hawapo tayari kuvumilia Rushwa kwa miezi sita  kama ilivyo ahidiwa na Makamu wake Mangula.

Sungura amesema kuwa wanatoa siku saba kwa CCM kuhakikisha kuiagiza Serikali yake kuikomesha  Rushwa na matendo yanayoendana nayo ndani ya siku saba kuanzia sasa.



"enzi za mwalimu Nyerere tulikuwa tunapata tabu sana kuwabaini wala rushwa  tofauti na sasa ambapo wala Rushwa wote wanajulikana", amesema Sungura
Chakushangaza baada ya Makamu mwenyekiti kuongea na kuonyesha jinsi alivyokerwa na Rushwa iliyopo katika CCM, Afisa habari wa chama hicho Bw, Florian Lutayigwa alianza kuwagawia Baadhi ya waandishi waliokuwemo katika mkutano huo shilingi 5000 kila mmoja  ambazo wengi tulitafsiri kwamba ni Rushwa ili waandishi wakaiandike habari hiyo kama ilivyo.

Na wakati akitoa pesa hizo alikuwa anawaambia waandishi hao kuwa wahakikishe wameandika story  kwani kesho atanunua magazeti kuona kama habari imetoka.



Hawa ni waandishi wa habari waliokuwemo kwenye mkutano huo

Hapa Bw, Florian Lutayigwa akitoa pesa kwa waandishi waliohudhuria katika mkutano huo

Majina ya waandishi watakaopewa shilingi 5000 yanakaguliwa

Chukua 5000, hakikisha habari imetoka

Fulani njoo uchukue 5000 yako

No comments:

Post a Comment