Kufuatia maelekezo ya TCRA
mfumo wa analogia utakoma kabisa kutumika hapa nchini Tanzania tarehe
31 Desemba, 2012. Baada ya tarehe hiyo mfumo rasmi wa utangazaji wa
matangazo ya televisheni utakuwa katika mfumo wa digitali. Kwa hali hiyo
watanzania wanaotumia mfumo wa analogia kwa sasa wanalazimika
kujiandaa mapema na mabadiliko hayo kwa kununua ving’amuzi au
televisheni za digitali katika maduka ya starTimes au kwa mawakala wetu
popote walipo nchini.
Ili kuweza kuingia mapema katika
mfumo mpya wa utangazaji wa television wa digitali, Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) lilingia ubia na kampuni kutoka China
ijulikanayo kama STAR COMMUNICATION NETWORK COMPANY LTD na kufungua
kampuni hapa nchini kwa pamoja iitwayo STAR MEDIA (TANZANIA) LTD kwa
jina la kibiashara StarTimes.
Wajibuwa kampuni ya StarTimes ni
kuanzisha mfumo mpya wa kurusha matangazo ya hewani kwa mfumo wa
digitali nchini Tanzania. Startimes kwa sasa inapenda kuwatangazia
wananchi upunguzaji wa bei zake kwa mfano; King’amuzi kimepungua bei kwa
asilimia zaidi ya 30 kutoka 70,000/= mpakakufikia 39,000/= katika
kusheherekea sikukuu hii ya Christmas kuanzia 15 November 2012 mpaka 31
January 2013. King’amuzi hicho kitakuwa na (warranty) udhamini wa mwaka
mmoja na kitapatikana maduka yetu yote ya startimes Tanzania ukijumuisha
namawakala wetu popote walipo.
Wateja pia wanaweza kuchagua
kifurushi wakipendacho, kwa kuwa kampuni hivi karibuni iliongeza chaneli
za ndani na za kimataifa katika orodha yake yavifurushi nakufikisha
idadi ya zaidi chaneli 54. Viwango vya malipo vimepangwa katika makundi
yafuatayo:
- Kifurushi cha MAMBO kwa TSh. 9,000/=, chaneli 30+
- Kifurushi cha UHURU kwa TSh. 18,000/=, chaneli 45+
- Kifurushi cha KILI kwa TSh. 36,000/=, chaneli 54+
Kwa sasa kampuni ya StarTimes
inaendelea na ujenzi wa vituo vipya vya kurusha matangazo ya digitali
katika mji ya Morogoro na visiwani Zanzibar na baadae mwaka ujao
itaendelea kufunga mitambo hiyo katika mikoa mingine. Kwa vituo
vilivyokwisha jengwa mpaka sasa ni katika miji ya Dar-es-salaam, Dodoma,
Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi naTanga.
Katika jitihada za kuwaburudisha
Watanzania kufurahia michezo kutoka dunia kote, StarTimes sasa inarusha
mechi nyingi na nzuri za Barani Ulaya kupitia chaneli ya DTV. Hata hivyo
Startimes itazindua ofa maalum ya Christmas itakayoanza tarehe 15
Novemba, 2012 hadi 31 Januari, 2013 kama ifuatavyo:
- Wateja wa zamani: Ukiongeza salio kwa miezi mitatu unazawadiwa mwezi mmoja bure.
- Kingamuzi: Ukinunua king’amuzi kimoja kwa TSh. 39,000/=, una uamuzi wa kuchagua kifurushi unachokitaka kati ya MAMBO, UHURU.
- TV ya digitali 21”CRT: Kutoka TSh. 285,000/= hadi TSh. 239,000/=, unapata pamoja na mwezi mmoja kifurushi cha Uhuru.
- TV ya digitali 24” LCD: Kutoka Tsh. 544,000/= hadi TSh. 449,000/=, unapata pamoja na mwezi mmoja wa kifushi cha Uhuru.
- TV ya digitali 32”LCD: kutoka shilingi 835,000/= hadi TSh. 699,000/=, unapata pamoja na mwezi mmoja kifurushi cha KILI.
- TV ya 42” LED: Unapata pamoja na king’amuzi kimoja bure kwa TSh. 1,300,000/=, ikijumishwa na mwezi mmoja wa kifurushi cha KILI.
Zawad izaidi zitatolewa kwa wateja wapya na wale wazamani.
Katika kusherekea sikukuu ya
Christmas StarTimes inawapa nafasi kubwa Watanzania wote kusherekea
sikukuu hii pamoja na familia zenu namarafiki hasa katika kipindi hiki
cha sikuu.
Kadri tarehe ya kufunga mfumo wa
analog inavyokaribia StarTimes imejitahidi kupunguza gharama zake za
huduma na bidhaa zake tofauti na makampuni mengine.
Mpaka sasa StarTimes ina wateja
wapatao million 7 duniani kote ambapo kwa Afrika inawateja wapatao
milioni 1.5 kwa nchikumi za kiafrika.Tanzania ni nchi mojawapo inayopata
huduma hii ya mfumo wa digitali kwa bei nafuu na wananchi kufurahia
thamani ya malipo yao.
Kwa taarifa zaidi tembelea madukaya StarTimes pamoja na mawakala wetu wa StarTimes popote walipo.
No comments:
Post a Comment