KATIKA kupunguza msongamano wa
magari jijini Dar es Salaam, Manispaa ya Ilala imewakamata Wamiliki 136
wa majengo ambao wamejenga bila kufuata sheria na kanuni za kuwa na
Maegesho maalumu katika majengo yao.
Hali hiyo imetokana na majengo
mengi kukosa maegesho hali inayosababisha wafanyakazi wa wanaofika
katika majengo hayo kukosa nafasi za kuegeshea mari hali inayowafanya
kuacha maeneo ambayo siyo rasmi, kuziba barabara nakusababisha foleni
zisizo za lazima.
Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi, jijini jana, Msemaji wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu
alisema watu hao wamekamatwa katika kipindi cha kuanzia Januari hadi
Oktoba mwaka huu.
Alisema wamiliki hao,
walikamatwa kutokana na kukiuka sheria inayowaagiza kila anayejenga
jengo lazima ahakikishe kuwa anajenga eneo la maegesho ya magari.
Tabu alisema baada ya wamiliki
hao kukamatwa walitozwa faini yenye thamani ya sh milioni 25 ambapo
miongoni mwao kuna waliokaidi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Alisema ili kuboresha operesheni
hiyo, Manispaa itatumia sheria na Namba 8, za mitaa ya mwaka 1982 na
kanuni ya mwaka 2008, ambazo zitatumiaka katika kusimamia na kuwabana
wale wote wanaokwenda kinyume.
Akifafanua zaidi, alisema
Manispaa hiyo ilitangaza zabuni ya kumpata wakala atakayesimamia kazi
hiyo mara baada ya kukamilia upembuzi yakinifu, ataanza kazi mapema
mwaka ujao.
Tabu alisema Manispaa hiyo
inatoa wito kwa kila anayetarajia kujenga jengo kuwa anahakikisha kuwa
anajenga maegesho ambayo yatatumika kwa ajili ya magari tu bila
kuchanganya na shughuli nyingine kinyume chake atafikishwa kwenye vyombo
vya sheria.
No comments:
Post a Comment