Friday, November 23, 2012

WAZIRI WA HABARI AFUNGUA KIKAO KAZI CHA SEKTA YA UTAMADUNI



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Kikao Kazi cha tisa cha Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini (hawapo Pichani).Kikao hicho kilifanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kauli mbiu ilikuwa ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe Chachu ya Maendeleo. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akisisitiza jambo kwa katika Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Kikundi cha Wasanii wa ngoma za asili ambacho kikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salam. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa  Kikao kazi cha tisa cha Sekta  ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaa. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini wakimsikiliza Wazari wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi  wa Kikao kazi cha tisa cha sekta hiyo kilichofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo. 
(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

No comments:

Post a Comment