Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.
Mpambano huo utafayika January
26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit)
katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!
Cheka na Chimwemwe watakutana
jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani
mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati
na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili
wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!
Mpambano wa Cheka na Chimwemwe
jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya
jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa
bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka
Chagga Boy!
Umaarufu wa wawili hawa
umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya
kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka
26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano
utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!
Katika tamasha hilo, pambano kuu
litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0 kutoka Marekani
ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana na bondia
Sammy Retta – 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF
Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa
juu (Heavyweight)
Mapambano mengine yatawakutanisha
mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia
Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea
ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG)
katika uzito wa Welterweight
Naye Manzur Ali 7(4)-8(3)-0
bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na bondia
Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki
ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light
heavyweight.
Mpambano huu umeidhinishwa na
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).
No comments:
Post a Comment