Ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Morogoro (SUA ), Mkaazi wa Njombe! Zawadi Nono Ya Fedha Taslimu, Shilingi Laki Tano ( Tsh.500,000/=) Za Kitanzania, kutolewa kwa mtu atakaye fanikishwa kukamatwa kwa tapeli hili la mtandaoni.
Hatimaye
yule tapeli sugu wa mtandaoni aliyekuwa akiwatapeli wananchi
mbalimbali kwa jina la RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia ajira
ajulikana .
INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013,
tuliripoti kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini
kuhusu kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia
jina la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya
huruma kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa
Zoom Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013
akitangaza nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali
mbali ya Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli
huyo
aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na
kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa
wamepata nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka
wamtumie
shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa kwenda namba 0763906931 (
AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU ).. Baada
ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza
kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja kati yao
akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu mara baada ya kutembelewa
na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo. Dada huyo aliye
jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni Muhitimu wa Chuo
Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika ofisi zetu siku ya
tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili
asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya kufanya naye mazungumzo
ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao fanyika kwa jina la
taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda kuripoti uhalifu huu kwenye
kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, na
kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI
KWA NJIA YA MTANDAO.
No comments:
Post a Comment