Naibu katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Bw, Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam. |
Chama cha wananchi CUF kimeendelea kutoa laana kwa vitendo
viovu vinavyotokea hapa nchini kama
ilivyo kawaida ya chama hicho kutoa laana kwa vitendo hivyo.
Leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo Naibu
katibu mkuu wa Chama Bw, Julius Mtatiro, hicho alikuwa akizungumza kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Chama hicho amesema kuwa CUF ina laani manyanyaso ya Polisi dhidi
ya Raia kama ilivyotokea hivi Karibuni Mkoani Kigoma,Tegeta jijini Dar es
Salaam, mauaji ya RPC Mwanza, Zanzibar na pia kujeruhiwa kwa waandishi wa
habari kwa Risasi kama ilivyotokea Mkoani Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Mtatiro amesema kuwa wanamtaka IGP
kuwachukulia hatua za Kinidhamu watendaji waliohusika na vitendo hivyo.
CUF pia imemtaka waziri wa Nishati na Madini Prf, Muongo
kuwaeleza Wananchi ninini Tatizo la kuendelea kwa Mgao wa Umeme kinyemela
wakati alikwisha Tangaza kuwa hakutakuwa na Mgao wa Umeme tena.
Aidha Mtatiro amesema kuwa
wanapinga mpango wowote wa kutaka kuongeza bei ya Umeme nabadala yake
wameitaka Serikali kutatua tatizo kwenye sekta ya Umeme ili watanzania Wote
wanufaike na Huduma hiyo.
MAASINDA, imejaribu
kutafuta mawazo ya watu wengine wanasemaje
juu ya Matamko yanayotolewa na CUF na kufanikiwa kupata ktoka kwa watu
mabalimbali ambapo wengi waliisifu kwa matamko yao lakini walitaka waone
Vitendo na Sio matamko peke yake.
Josephat Jacob, ni
mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa CUF kwa mara nyingi wamekuwa wakilaani
vitendo viovu vinavyo fanywa na Serikali ya CCM lakini hamna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya matamko
yao na CUF wanaona kuwa hawajasikilizwa lakini hawachukui hatua zozote.
“Tunataka kuona CUF wanachukua hatua kwani wao wana nafasi
ya kusema na kutenda sio wanasema tu, wanalaani tu, na kutoa matamko halafu
yasipofanyika wanabaki kimya wanasubiri waseme tena ndipo watoe Tamko na Kulaani
tumechoshwa na Siasa zao”, amesema Jacob.
Naye Erick Kivuyo wa Buguruni Dar es Salaam amesema
kuwa Wanataka kuona kuwa hatua
zinachukuliwa na sio maongezi tu ya
kuwaridhisha watanzania.
“Maneno Mengi hayavunji Mfupa watanzania Tunataka kuona jambo
linaongelewa na linatendeka sio kuzungumza tu wakati maneno mengi hayavunji
Mfupa”, amesema Kivuyo.
Waandishi wa Habari waliokuwemo kwenye Mkutano huo |
Hawa ni viongozi wa CUF waliokuwemo kwenye Mkutano huo |
No comments:
Post a Comment