Saturday, December 22, 2012

WAZIRI WA HABARI DK MUKANGARA ALIPOTEMBELEA OFISI ZA TBC MWANZA


Mhandisi Zablon Mafuru (kulia) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mwanza  akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kulia) hivi karibuni mtambo wa redio Tanzania wa masafa marefu (Medium Wave) unaorusha matangazo yake katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Kigoma , Siminyu  na nchi jirani za Uganda na Rwanda uliopo Ilemela jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akiangalia mtambo wa kurushia matangazo ya redio kwa  masafa mafupi  (Short Wave) na Televisheni wa Shirika la Habari la Tanzania (TBC) hivi karibuni uliopo eneo la Nyashana jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akikagua hivi karibuni kiwanja cha Shirika la Habari la Tanzania (TBC) kilichopo  eneo la Kapripointi jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (wa pili kulia) akiongea jambo hivi karibuni na  baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Habari la Tanzanzani (TBC) mara baada ya kumaliza ziara yake fupi ya kutembelea ofisi za kanda ya Ziwa za shirika hilo zilizopo jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo na wapili kushoto ni  Mhandisi Zablon Mafuru ambaye ni mkuu wa Kituo cha Mwanza akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka  Idara ya Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi  (aliyevaa suti ya dark blue).
Mhandisi Zablon Mafuru (kulia) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa pili kulia) mtambo wa kurusha matangazo Televisheni kwa njia ya digitali (haupo pichani) uliopo eneo la Nyashana jijini Mwanza. Kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka 2013 vituo vyote vya Televisheni vitarusha matangazo yake kwa njia ya digitali.
  Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment