Friday, December 7, 2012

IDARA YA UHAMIAJI WAFANYA SEMINA KUHUSU ANUAI ZA JAMII, WATANZANIA WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Nchini Bi, Salome Kahamba akizungumza katika semina ya Siku mbili iliyoanza jana jijini Dar es Salaam inayohusu anuai za jamii ikiwemo UKIMWI, na unyanyasaji ambapo alisema kuwa Changamoto wanayoipata kubwa wao kama Idra ya uhamiaji ni Kwamba watu hawataki kupima UKIMWI ili kujua Afya zao ambapo amewataka Watanzania wapime Afya zao ili waweze kujijua mapema na kujipatia Dawa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Warsha hiyo iliyoanza jana katikaHoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam akisoma hotuba yake ambapo alisisitizakuwepo kwa Elimu kwa wazee baada ya kustaafu, aliwataka pia watanzania Kupima Afya zao na kuchukua majibu ili waweze kujigundua kuwa wapo salama au la, na kama hawatakuwa salama waaanze kutumia Dawa mapema.

Hawa ni Wadau waliohudhuria katika  Warsha hiyo

Kikundi cha ngoma kikitoa Burudani katika Warsha hiyo ambapo Mgeni rasmi alifurahishwa sana na Burudani hiyo na hata akaamua kutoa zawadi yapesa kwao

Walipokuwa kwenye picha ya Pamoja

Mgeni Rasmi anaongea na waadishi wa habari

Mgeni Rasmi akitoa kiasi cha shilingi laki moja na elfu tano kwa kikundi cha ngoma

Nahakikisha pesa Mheshimiwa

Zipo sawa..... Nashukuru Mheshimiwa

No comments:

Post a Comment