Friday, December 21, 2012

JUKWAA LA KATIBA LASEMA NI NDOTO KATIBA MYA KUPATIKANA 26 APRIL 2014

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) juu ya Uharakishaji wa Mchakato wa Katiba ambapo amesema kuwa unaanza kuleta Fujo na kuathiri ushiriki wa Wananchi katika uundaji wa Katiba mpya.
Bw, Kibamba amesema kuwa,  kuna makundi maalumu  ambayo yananyimwa haki ya kushiriki katika kutoa michango yao katika mchakato wa Katiba Mpya, ambapo ametaja baadhi ya makundi hayo kuwa ni Kundi la watu wenye ulemavu wasioweza kusikia na kuongea wanaoshindwa kutoa maoni kwa kukosa wakalimani wa lugha ya Alama, ambapo amesema kuwa hata matangazo yaliyotolewa kupitia Redio na Televisheni yameshindwa kuwafikia watu wenye Ugumu wa Kusikia.

Jukwaa la Katiba limependekeza kuwa Matangazo yote ya Kwenye Luninga yapatiwe wakalimani/ wafasili wa lugha ya Alama ili wasiosikia pia waweze kufwatilia kupitia Runinga.

Kibamba amelitaja kundi lingine ambalo halijatendewa haki na Tume ya Katiba kuwa ni Watanzania walioko Magerezani wakiwa kama wafungwa au mahabusu.

"Kundi hili limenyimwa haki kwa Miaka Mingi sana, Jukwaa la Katiba tuliwafikiria mapema, na tulitaka tupate Ruhusa ya Magereza ili tukakusanye Maoni yao lakini tuliahidiwa kuwa Tume itakusanya maoni yao ila mpaka sasa Tume imemaliza mchakato wa Kukusanya Maoni pasipo kukusanya maoni ya Wafungwa", amesema Kibamba
Jukwaa la Katiba limezidi kusisitiza kuwa hawana imani kwamba Mchakato wa Katiba utakamilika ifikapo 26 Aprili 2014 kutokana na Mapungufu yaliyopo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba akionyesha Baadhi ya Katiba ambayowameibuni inayoweza kutumiwa na watu wasio ona


Jukwaa la Katiba pia linatoa vyeti kama Adhabu kwa watu wanaokwamisha mchakato wa Katiba Mpya na Nakala ya Vyeti hivyo inapelekwa Kwa Rais Jakaya Kikwete mpaka sasa tayari wametoa vyeti kwa  Mbunge Rosmary Kirigir pamoja na DC Kasunga

Hichi cheti cha DC Kasunga
Tume ya katiba imetakiwa Kuwatendea haki wananchi wote wa Tanzania katika kutoa maoni yao la sivyo Jukwaa la Katiba litawapa Cheti  cha kuwatambulisha kuwa wao ni Maadui wa Katiba mpya.

No comments:

Post a Comment