Tanzania
Bara (Kilimanjaro Stars) itacheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la
Chalenji 2012 Alhamisi (Desemba 6 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mandela
ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda.
Kilimanjaro Stars ambayo itacheza mechi hiyo na mshindi wa robo fainali
ya kesho (Desemba 4 mwaka huu) kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia
imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Rwanda. Mechi imechezwa leo (Desemba
3 mwaka huu) Uwanja wa KCC ulioko Lugogo, Kampala.
Mabao ya Amri Kiemba dakika ya 33
na John Bocco dakika ya 53 ndiyo yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge
nusu fainali na kuifungisha virago Rwanda (Amavubi) inayofundishwa na
Milutin ‘Micho’ Sredojovic kutoka Serbia.
Vijana wa Kilimanjaro Stars
wanaonolewa na Kim Poulsen walitawala pambano hilo, hasa kipindi cha
kwanza kwa pasi fupi fupi. Kilimanjaro Stars imefungwa bao moja katika
mechi nne ilizocheza tangu michuano hiyo ilipoanza Novemba 24 mwaka huu
jijini Kampala.
Kilimanjaro Stars ambayo katika
michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana iliishia hatua ya
nusu fainali iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah,
Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athuman
Idd, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngasa.
No comments:
Post a Comment