Mahmoud Ahmad Arusha
Matukio ya ubakaji watoto wadogo
yameendelea kujirudia mkoani hapa baada ya mtoto wa miaka miwili aitwaye
Stela Jacob mwenye umri wa miaka 2 na nusu mkazi wa Ilboru kubakwa
hadi kulazwa kwenye hospitali ya mkoa ya mount meru jijini hapa.
Tukio hilo la kutisha limetokea
juzi majira ya asubuhi kwenye mtaa huo wa Ilboru kwa kijana wa miaka 20
nae ni mkazi wa mtaa huo kufanya kitende hicho cha kinyama baada ya
mama wa mototo huyo kutoka na kumuacha mtoto huyo akicheza na wenzake na
ndipo mtuhumiwa huyo kuamua kujifanyia anavyotaka kwa mtoto huyo,
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali
ya mkoa mama wa mtoto huyo aitwae Mariam Miller mwenye umri wa miaka 30
alisema kuwa yeye alipotoka kidogo kumsindikiza jirani yake aliporudi
alimkuta mtuhumiwa akiwa anavaa suruali baada ya kumaliza kitendo hicho
huku mtoto wake akilia kwa nguvu hali iliyomshitua na ndipo alipoamua kumuuliza mtuhumiwa.
Baada ya Mtuhumiwa kuulizwa na mama huyo, alitimua mbio bila ya kutoa majibu.
Baada ya Mtuhumiwa kuulizwa na mama huyo, alitimua mbio bila ya kutoa majibu.
Alisema kuwa alipo mkagua
alimkuta mwanae anamabaki ya mbegu za kiume kwenye sehemu zake za siri
na ndipo alipowaeleza nduguzake waliomshauri kumpeleka hospitali kwa
matibabu.
Walimpeleka hospitalini hapo kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupewa huduma wauguzi hospitalini hapo walimtaka apeleka PF3 ya polisi na ndipo alipotoa taarifa polisi.
Walimpeleka hospitalini hapo kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupewa huduma wauguzi hospitalini hapo walimtaka apeleka PF3 ya polisi na ndipo alipotoa taarifa polisi.
Wakati waandishi wakiendelea
kumuhoji mama huyo walipata taarifa za mtoto mwingine wa kike aitwaye
Zam zama Joseph mwenye umri wa miaka 10 aliyebakwa na kijana wa miaka 30
wote wakazi wa mtaa wa Pangani kata ya kati jijini hapa na kesi yake
ipo polisi kwa uchunguzi.
Nae kamanda wa polisi Liberatu
Sabas alisema kuwa jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi
wa matukio hayo na kuwa watuhumiwa wote wakikamatwa watafikishwa kwenye
vyombo vya sheria ili sheria ichukuwe mkondo wake na kuwataka
wakinamama kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kubaini au kukabiliana
na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment