Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi
wakati alipofungua rasmi Jengo la Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya
Kinyonga,wilayani Kilwa jana wakati wa kilele cha ziara yake ya siku
tano ya kikazi Mkoani Lindi.Kulia aliyesimama ni Mganga mkuu wa
Hospitali hiyo Dkt.Mike Mabimbi.
Mganga
mkuu katika hospitali ya Kinyonga,wilayani Kilwa Dkt.Mike
Mabimbi(kulia) akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda
mfupi baada ya Rais kufungua jengo la wazazi katika hospitali hiyo na
kulikagua.Wodi hiyo ya Wazazi imejengwa ikiwa ni Mkakati wa kuboresha
huduma ya Mama na mtoto Tanzania na ujenzi umefadhiliwa na Halmashauri
ya Kilwa pamoja na Chama Cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama
Tanzania(AGOTA) na shirika la Uholanzi la Bioshape Benefit Foundation.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa hadhara mjni Kilwa Kivinje,mkoani Lindi jana
jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi mjni Kilwa Kivinje
jana jioni.Rais Kikwete aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku tano
Mkoani Lindi amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.(picha na Freddy
Maro).
No comments:
Post a Comment