Baraza lilipitia malalamiko yote
na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki
katika mgomo huo. Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo,
onyo kali na kusimamishwa udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na
miezi sita.Vile vile kuna Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki
katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.
MCHANGANUO WA ADHABU
- Waliofutiwa mashitaka madaktari 49
- Waliopewa onyo madaktari 223
- Waliopewa onyo kali madaktari 66
- Kusimamishwa kwa muda madaktari 30
- Mashitaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria madaktari 4
- Mashitaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza madaktari 22
Wizara inakamilisha taratibu za
kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote
waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari.
Wizara pia imeridhia kuwapa Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa
vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za
Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa. Hata hivyo fursa hii haitawahusu
Madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari,
hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
HITIMISHO
Kwa taarifa hii madaktari wote
waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa
kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua
kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa
usajili na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo. Vile vile
madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Afya ili kupewa barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.
Barua hizi zitatolewa kuanzia tarehe 2 Januari, 2013.Madaktari wote
walio katika mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kuanza kazi katika vituo
vyao vya awali ifikapo tarehe 14 Januari, 2013.Hakuna muda utakaoongezwa
kwa kipindi kilichobakia cha mafunzo kwa vitendo. Kwa wale wote
waliopewa adhabu wataanza kutumikia adhabu hizo kuanzia tarehe ya adhabu
hiyo ilivyotolewa.
Nsachris Mwamwaja
Msemaji
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/12/2012
No comments:
Post a Comment