Waraka wa marekebisho ya Katiba ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umepita baada ya kuungwa
mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura.
Jumla ya wajumbe waliopiga kura
kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati
waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa,
hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya
marekebisho kikatiba.
Kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46, wajumbe kutokavyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni kumi na moja.
Kamati ya Utendaji ya TFF
inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono na
waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba.
Vipengele vilivyoingizwa ni ‘club
licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya
Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile Kamati ya Utendaji
itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za
Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya
Rufani ya TFF.
Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia
utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa
mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano
Mkuu siku 60 kabla.
No comments:
Post a Comment