Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akiangalia kahawa katika shamba darasa inayolimwa na Ibrahim
Mulokozi (kulia) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba
aliyenufaika na mkopo wa shilingi laki nne kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea shamba hilo la kahawa na
migomba jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kutoka SACCOS
ya Ibwera zimewanufaishaje kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akimuangalia samaki mwenye umri wa miezi mitatu anayefugwa
katika bwawa la Kikundi cha Msifuni kilichopo kijiji cha Kemondo
wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea bwawa hilo jana ili kuona
fedha za mkopo walizozipata vijana kupitia mfuko wa Halmashauri
nimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa tatu
kulia) akiangalia jana nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni
kilichopo katika kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata
mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la
samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Johanes Joel.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba
kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo
ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera
na viongozi wa wilaya ya Bukoba wakati alipowatembelea jana ili kuona
fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya vijana zilivyoweza
kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
akiangalia shamba darasa la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha
Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim Mulokozi (hayupo pichani) wakati
alipolitembelea jana ili kuona fedha za mkopo wa mfuko wa vijana
alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje kimaisha. Kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment