Goli
pekee la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC, limeipa ushindi
timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya SOFAPAKA uliochezwa jana
Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.
Azam FC imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki, juzi jioni walifungwa 2-1 na AFC Leopard katika mechi iliyochezwa uwanja huo.
Katika mchezo huo, kipindi cha
kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka suluhu, wachezaji wa Azam FC
Himid Mao alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba na kurudi ndani
katika dakika ya 14, dk 22 Seif Abdalah akiwa na lango la SOFAPAKA
alipiga mpira uliotoka nje.
Azam FC waliendelea kufanya
amshambulizi katika lango la SOFAPAKA, dk 27 na 45 Michael Bolou alipiga
shuti likatoka nje na dakika ya 37 Humprey Mieno alishindwa kufunga na
badala yake shuti likaokolewa na kipa wa SOFAPAKA, Duncan Ochieng
SOFAPAKA dk 24 Kago Dawson
alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti lililodakwa vyema na kipa
chipukizi wa Azam FC, Aishi Salum ambaye aliweza kulinda lango hilo
katika vipindi vyote.
No comments:
Post a Comment