Wednesday, January 9, 2013

KUBADILISHA LESENI MPYA ZA MADEREVA MWISHO NI MACHI 31 MWAKA HUU


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
…………………………………………………………………
Na Mobini Sarya, Tanpress
JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Mamlaka mapato nchini (TRA) limeboresha mfumo wa utoaji leseni za udereva ambazo zimeanza kutolewa kwa njia aya Smart Card ili kuendana na ukuaji wa Teknolojia duniani.
Wakizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mnadhimu  wa kikosi cha usalama barabarani ACP Johandani Kahatano na Naibu Kamishna wa TRA Yusuph Salum wamesema kuwa mwisho wa kubadilisha leseni kwa maedeleva wote ni Machi 31 Mwaka huu.
Wameeleza kuwa baada ya muda huo zoezi la ubadilishaji Leseni za aina zote halitafanyika na mfumo wa utoaji Leseni utabadilishwa ili kubakia na uwezo wa kutoa Lesseni kwa madereva wanaoomba Lesseni kwa mara ya kwanza.
Hivyo madereva wote wametakiwa kuhakikisha wanatumia muda huo wa miezi mitatu iliyotolewa kubadilisha Leseni zao ili kujiepusha na usumbufu unaoweza kuwapata.
Aidha Kamanda Kahatano amesema kuwa Dereva atakayekutwa anaendesha gari wakati leseni yake imekwisha atafikishwa mahakamani pamoja na mmiliki wa gari hilo.
     Zoezi la kutoa leseni mpya za udereva lilianza Oktoba Mosi  Mwaka 2010 kwa awamu ya kwanza iliyohusisha mikoa (9) na machi 2011 mikoa mingine 13 ilianza kutoa leseni hivyo zoezi hilo kukamilika.
Kamanda huyo amesema kuwa madhumini ya zoezi hilo ni kubadili mfumo huo na kuondoa tatizo la kughushi pamoja na kudhibiti mienendo ya madreva kwa kutunza kumbukumbuku za makosa yao.
Hadi kufikia Disemba 31 Mwaka jana leseni 616,349 zilizokuwa zimetolewa kwa nchi nzima ambapo kati ya hizo leseni 135721 ni za kundi lenye madaraja C zingine 480,628 ni za makundi mengine.
Hata hivyo takwimu hizo zikilinganishwa na idadi ya vyombo vya moto vilivyosajiliwa na Mamlaka ya TRA nchini hadi kufikia Disemba 2012 vinafikia 1,164,574 hiyo inaoonyesha kuwa kuna madereva wanaoendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na leseni halali.

No comments:

Post a Comment