Mwandaaji wa Mashindano ya Marathon
ya Kilomita 10 ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Sarah Ramdhani
ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania
kwa miaka 10 ambapo amewashukuru Mohammed Enterprises Tanzania Ltd
(MeTL GROUP) Kwa kudhamini mashindano kama haya kwa sababu miaka ya
nyuma yalikuwa yakikosa udhamini wa kuaminika na kwa mshangao wa wengi
walikua wakijua Mohammed anadhamini Soka tu lakini hawajui kwamba
hachagui na anadhamini michezo yote.
Kutokana na udhamini wake sasa
tumepata mahali pakujenga uwanja wa Riadha kwa sababu Uwanja wa Taifa
sasa umekuwa kama uwanja wa maonyesho wa soka lakini riadha tunakusudia
kujenga Pwani.
Mwandaaji huyo amemshukuru mdhamini
wa michezo hiyo na kusema kwamba wao kama chama watatimiza malengo ya
chama hicho kuitangaza Tanzania Kimataifa katika riadha.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania
Bw. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameshukuru
ubunifu huu wa kuazimisha mkesha wa mwaka mpya kwa aina tofauti ambapo
watu wengi wamezoea kuadhimisha katika kumbi mbalimbali za burudani
lakini sisi tumeadhimisha mwaka mpya kimichezo zaidi kwa kufanya
Marathon ya Kilometa 10 yaliyojulikana kama MeTL New Years Eve Midnight
Race.
Sisi kama wanamichezo tumekubaliana
na wazo hili la kufanya Marathon kama hii na tumashukuru MeTL GROUP kwa
kudhamini kitu kama hichi cha kipekee n kuwataka washiriki wajitokeze
kwa wingi mara nyingine na pia huu usiwe mwisho bali uwe ni mwanzo wa
kuendeleza michezo Tanzania na tunakiomba chama cha Riadha RT
kushirikiana na wadau wa michezo kukuza mchezo wa riadha Tanzania.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania
Bw. Anthony Mtaka akiambatana na viongozi wa chama cha riadha Tanzania
RT kuelekea kuzindua rasmi mashindano ya riadha ya Kilomita 10
yaliyofanya maeneo ya Masaki jijini Dar na kumalizika katika Polisi
Officers Mess.
Washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania wakiwa wamejipanga tayari kuanza mbio za Marathon 2012 katika
mkesha wa mwaka Mpya jijini Dar es Salaam.
On your Mark...........Get
Ready.......Paaaa..... Mgeni rasmi Bw. Anthony Mtaka aliyenyanyua mkono
juu kufyatua baruti kuashiria kuanza rasmi kwa mbio hizo huku washiriki
nyuma yake wakijipanga kushindana vilivyo.
Mshindi wa kwanza katika mbio hizo kwa upande wa Wanaume Bw. Dickson Marwa akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa 29:14:45.
Baadhi ya washiriki wengine
wakimaliza ngwe ya mashindano hayo ya Kilometa 10 yaliyomalizika katika
bwalo la polisi Masaki Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania L.t.d (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akichezea
ngoma za asili ya kabila la Wagogo sambamba na Watumbuizaji hao wakati
wa mashindano ya riadha ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' usiku wa
mkesha wa Mwaka mpya 2013 yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo Masaki
jijini Dar.
Pichani juu na chini washiriki walifanikiwa kumaliza mbio hizo wakijiandikisha.
Joggers wakiingia katika viwanja vya
Police Officers Mess baada ya kumaliza ngwe yao katika mashindano hayo
ya mbio za kilomita 10 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL GROUP) katika mkesha wa kuukaribisha
mwaka mpya 2013 usiku wa kuamkia leo.
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo Bw.
Said Abrahman kutoka Zanzibar akiwa amezinduka baada kuzimia alipo
maliza ngwe hiyo katika viwanja vya Police Officers Mess jijini Dar es
Salaam.
Meza Kuu...Mwakilishi kutoka kampuni
ya MeTL GROUP Bw. Cosmas Mtesigwa akiteta jambo na Rais wa Chama cha
Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka kabla ya kuanza kwa zoezi la
kutoa zawadi kwa washindi.
Pichani juu na Chini ni Baadhi ya
washiriki wa Marathon wakicheza kwaito na kufurahia baada ya kutimia
saa 6 kamili na kuuona mwaka Mpya 2013.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah
Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha
Tanzania kwa miaka 10 akiwa na waratibu wengine wa shindano hilo
wakiratimisha shindano hilo ili kujua kuweza nani amepata pointi zipi na
kuweza kumtangaza mshindi halali.
Pichani Juu na Chini ni Mgeni rasmi
Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiongoza
washiriki mashindano ya riadha na wageni waalikwa kupata chakula cha
jioni kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Rais Mstaafu wa Chama cha Riadha
nchini (RT) Bw. Francis John akitoa nasaha kwa washirki ambapo amewataka
kuongeza juhudi zaidi na kutokata tamaa kwa kuwa michezo ni Afya na
kuwaasa wananchi wengine zaidi kujitokeza pamoja na wadhamini wengine
katika tukio kama hili ili kuupa kipaumbele mchezo wa Riadha kama
ilivyoonyesha mfano na kampuni ya MeTL GROUP.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah
Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha
Tanzania kwa miaka 10 akiwatolea uvuvi viongozi wa vyama vya michezo vya
sasa kuwacha kula kwenye michezo ya wanamichezo na kujikita katika
kuvumbua vipaji vipya kwa sababu tumekuwa tukiwaona walewale kila siku
kwa kufanya hivyo mtakuwa hamkuzi mchezo huu.
Mwakilishi wa Kampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akizungumza
kwa niaba ya Kampuni ambapo imeahidi kuendelea kushirikiana na wabunifu
wa michezo hii na pia kuendelea kushirikiana nao bega kwa bega mpaka
kufikia michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Brazil na kuhakikisha
wanapata medali na kuipatia sifa nchi yetu kwa kuwa na wanamichezo bora.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania
(RT) Bw. Anthony Mtaka akiwaasa washiriki na kutoa shukrani za pekee kwa
Kampuni ya MeTL GROUP kwa kuelekeza macho nguvu zao kusapoti mchezo wa
riadha ambao umekuwa haupewi kipaumbele na wadhamini wengine ambao
wamekuwa wakitazama mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingineyo.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya
kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa
wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bw. Dickson
Marwa aliyemaliza katika muda wa dakika 29:14:45 zilizodhaminiwa na MeTL
GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa
Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi
kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya
kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa
wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bi. Sara
Ramadhani aliyemaliza katika muda wa dakika 33:02:31 zilizodhaminiwa na
MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited. Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa
Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi
kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa akikabidhi
zawadi ya kitika cha Shilingi 100,000/= kwa Mshindi wa tatu kwa jamii
ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Mathia Jolo
aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 43:16:07 yaliyofanyika
katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es
Salaam
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya
kitika cha Shilingi 500,000/= kwa Mshindi wa pili kwa jamii ya watu
wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Shukuru Khalfan
aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 38:51:10 yaliyofanyika
katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es
Salaam.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikata keki ya
kuukaribisha na mwaka 2013 baada ya kukabidhi zawadi kwa washiriki wa
Marathon za Mbio za Kilometa 10 usiku wa kuamkia leo jijini Dar.
MgeniRais wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akifungua rasmi muziki kwa wote baada ya
zoezi la kukabidhi zawadi.
No comments:
Post a Comment