Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA aliyesimamishwa hivi karibuni leo ameinuka na
kuyasema yake ya Moyoni kuhusiana na Kusimamishwa kwake na pia akayasema machafu yaliyomo katika
Chama hicho.
Akizungumza
leo
katika Mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika jijini Dar es
Salaam, Bi Juliana Shonza ameseme kuwa yeye hajapewa barua ya
kufukuzwa uanachama kwa hivyo bado anajua
kuwa yeye ni Mwanachama wa Chadema na ni Makamu mwenyekiti wa BAVICHA.
Bi Shonza ametumia nafasi hiyo kuyasema yanayofanywa
ndani ya Chama hicho ambayo alikuwa anapingana nayo mara kwa mara ambapo
anasema kuwa alikuwa anapinga kitendo cha Mwenyekiti wa Chama hicho kufumbia
macho Katibu mkuu wa Chama hicho
kujikopesha pesa za Ruzuku ya chama kiasi cha Shilingi milioni 140 kwa manufaa yake binafsi ambapo hajazilipwa
mpaka leo.
Aliendelea kusema kuwa
alikuwa anashauri uongozi wa Chama hicho kuwa na Jengo la chama na
kuondokana na Kupanga, jambo ambalo linakifanya Chama kulipa mamilioni ya pesa
kwa ajili ya kulipa kodi ya Jengo la makao makuu, kwani Chama kina uwezo wa
kuwa na majengo yake yenyewe.
Aidha Juliana ametaka Mshahara wa katibu mkuu wa Chama
hicho Dk Willibord Slaa ambao ni zaidi
ya Milioni saba kwa Mwezi ambao unaambatana na Marupurupu kibao ili pesa hizo
na mamilioni zielekezwe kujenga chama mikoani.
“Namshangaa mwenyekiti kudai madai yangu ni ya kitoto
sasa sijui ni madai yapi anayoyazungumzia ni yapi? Na je ni haya ya mimi kudai
vitu vya Msingi”, amesema Juliana Shonza.
Hapa wakizungumza na waandihi wa habari |
No comments:
Post a Comment