Wednesday, January 9, 2013

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA TIGO TIME

Mbunifu wa ofa za Tigo,  Bi. Jacqueline Nnunduma akitambulisha huduma mpya ya Tigo ijulikanayo kama Tigo Time, mbele ya waandishi wa Habari (hawapo Pichani) leo jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo inatoa punguzo la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7) ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa. Pembeni ni Mwakilishi wa Kampuni ya Frontline, Bw. Elias Bandeke.
Meneja Mbunifu wa Ofa za Tigo Tanzania,Suleiman Bushagama (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mbunifu wa ofa za Tigo, Jacqueline Nnunduma na Katikati ni Mwakilishi kutoka Kampuni ya FrontLine, Elias Bandeke ambao ni Waratibu wa Mkutano huo.
Waashishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
Waandishi  wa habari pamoja na wapiga picha wakifuatilia kwa makini Mkutano huo.(Picha zote na Kajunason Blog)
---
Tigo imetambulisha huduma mpya kwa wateja ujulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.

Kusajili huduma kwa mteja piga *149*90# au tuma neno “TIGO TIME” kwenda namba “15372” na baada ya hapo utapokea ujumbe ambao utaonyesha kwamba umefanikiwa kusajili na unaweza kuanza kutumia huduma hii na ufurahie punguzo kubwa sana la gharama. Baada ya kusajili, Tigo Time itakujulisha punguzo lako la gharama la kupiga simu kutokana na muda wa siku na eneo ulipo. Gharama ya huduma hii ya kusajili itakuwa ni Tshs 149 kwa kiwango cha chini.

“Tigo inatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu na hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa juu na vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda wowote.” Alisema Bi. Jacqueline Nnunduma, Mbunifu wa ofa za Tigo. “Kwa punguzo hili kubwa la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo Time itakuwa huduma maarufu kama ilivyokuwa huduma ya ya Kwa Sekunde tuliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.” Alimalizia Bi. Nnunduma.

No comments:

Post a Comment