Thursday, January 3, 2013

TMA WATOA UTABIRI KWA KIPINDI CHA JANUARY HADI MACHI 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dk Aggness Kijazi akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari leo katika makao makuu ya Ofisi hizo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania  TMA imetoa taarifa kwa Umma kuhusu hali ya mvua nchini kutoka na utabiri uliofanywa na Mamlaka hiyo kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa Mamlaka ya hali ya hewa Nchini katika msimu wa wa Octoba hadi Desemba 2012 maeneo Mengi yalitarajiwa kuwa na Mvua za Wastan ambapo utabiri huo ulihusu zaidi maeneo yanayopata Mvua mara M,bili kwa mwaka ambayo ni Kanda ya Ziwa  Victoria  nyanda za juu kaskazini Mashariki na Pwani ya Kasklazini.

Dk Kijazi amesema kuwa Katika Kipindi cha Mwezi January hadi March 2013 kunatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya Wastani isipokuwa maeneo ya Kaskazini Mangaribi ambayo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya Wastan..

No comments:

Post a Comment