Thursday, January 3, 2013

TCRA YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KWENYE MFUMO WA DIJITALI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prf John Nkoma akizungumza na waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa Mikutano katika makao makuu ya Mamlaka hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imeahidi kufwatilia kwa makini Changamoto zilizopo katika mfumo huu mpya wa Digitali pamoja na Kuzitatua kwa haraka ili wateja wafaidi huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mkuu wa  TCRA Prf John Nkoma amesema kuwa, TCRA sasa inajielekeza kutatua changamoto zinazotokea baada ya Kuhamia kwenye mfumo wa Matangazo ya Televisheni ya Dijitali kama Inavyoripotiwa kila siku.

Amezungumzia Bei ya Vin'gamuzi kuwa imeshuka baada ya Serikali kupunguza Kodi kwenye Vingamuzi hivyo hivyo kila mwananchi ataweza kujipatia Kin'gamuzi.

"Mamlaka inafwatilia kwa karibu huduma zinazotolewa  na makampuni yote yaliyopewa Leseni ya kuuza Ving'amuzi na tumewaagiza watoa huduma kuboresha huduma zao kwa kuongeza Maduka ya kuuzia Vin'gamuzi", amesema Prf Nkoma.

Ameongez kuwa Vituo vyote vya Utangazaji  wa Luninga ambavyo havuijajiunga kwenye mfumo wa Dijitali kufanya hivyo Mapema ili Wananchi wafaidi huduma zao.
Prf Nkoma kulia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kushoto ni Meneja mawasiliano wa TCRA Bw, Innocent Mungi

Baadhi ya waandishi wa Habari waliokuwemo kwenye mkutano huo

No comments:

Post a Comment