Friday, January 4, 2013

Uharibifu wa mvua kubwa wailazimu TRL kusitisha safari za treni ya mikoani



 
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimelazimu Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) kusitisha kwa muda safari za treni zinazokwenda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara zikitokea jijini Dar es Salaam.

Mvua hizo zimeharibu sehemu kubwa ya tuta la njia ya reli lililoopo katika eneo la Mikese, Morogoro.

Afisa uhusiano wa TRL, Midladjy  Maez amesema bado haifahamiki safari zitarejea lini kutokana na kukabiliwa na tatizo la malighafi ya kukarabati eneo hilo.

“Hadi sasa hivi tunasubiri taarifa za wataalamu wetu ambao wako kule wanafanya tathmini hii njia itatengemaa saa ngapi na labda taarifa za uhakika zitatolewa kesho… tunahitaji kusafirisha mawe makubwa kutoka Dodoma yaletwe Morogoro, itachukua muda kidogo...” alisema Maez.

No comments:

Post a Comment