Umoja wa Vijana wa CUF umesema kuwa wanawaunga Mkono kwa
asilimia zote Wananchi wa Mtwara kwa
kuandamana kupinga Gesi kupelekwa Dar es Salaam kwani ni haki yao ya msingi
kwani Gesi ikifika Dar es Salaam Wananchi wa Mtwara hawatafaidika na chochote.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa UVICUF leo alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari katika makao makuu ya Ofisi hizo
jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa wanahitaji Ujenzi wa ku Vinu vya kufulia Gesi ufanyike
Mtwara ili kukuaza maendeleo katika
mikoa ya kusini ambapo vijana watajipatia ajira.
Amesema kuwa, kuisafirisha Gesi kuja Dar es Salaam
kutawafanya Wanamtwara kuiacha Mtwara na kuja kuongeza watu Dar es Salaam
badala ya kubaki kwao na kufaidika na Ugunduzi wa Gesi kwao.
“Ni haki ya Msingi kabisa wananchi wa Mtwara kuandamana kupinga Gesi kupelekwa Dar es
Salaam wakati hawajui hatma yao”
amesema Katani.
No comments:
Post a Comment