Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa
Ving’amuzi vya DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka
walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani
City jijini Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini
Afrika ya Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha
bahati nasibu kwa wapenzi hao wa Soka walikuwepo hapo.Kushoto ni Meneja
Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja
Mahusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati
nasibu ya Shinda King’amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano
ya Kombe la Afrika.
Meneja
Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto)
akikabidhi King’amuzi hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyi,ambaye ni
Mwanalibeneke wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh…..!! jamaa anazali huyu!).
Baadhi
ya Wadau wa DStv wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa
ya Afrika,kati ya timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao
ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.
Wadau
kibao toka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha
Samaki Samaki jijini Dar kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea
nchini Afrika ya Kusini yanakofanyika Mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment