Jengo la Coco Plaza ambalo kuna Ofisi za CRDB.
Wateja wakipata huduma.
Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei
Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei
(kushoto) akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi
hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai. Tawi hilo
limefunguliwa hivi karibuni katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Nasib Kalamba.
Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba (katikati) akitoa ufafanuzi
kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai
kaatika tawi jipya la benki hiyo lililopo katika jengo la Coco Plaza
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo, Godlisten
Mtei.
Ofisa wa benki ya CRDB, JacqlineSawe akitoa maelekezo kwa mteja wa benki
hiyo katika tawi la Oysterbay lililopo katika jengo la Coco Plaza
jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib
Kalamba (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa
zamani wa Elimu, Joseph Mungai katika tawi jipya la Oysterbay jijini Dar
es Salaam.
Wateja wakipata huduma.
Maofisa wa benki ya CRDB wakiandisha wateha wapya katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei (kushoto) akitoa maelekezo
ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai.
Ofisa wa benki ya CRDB, George Abraham kisaini baadhi ya nyaraka za kibenki.
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya CRDB, imefungua tawi jipya Osysterbay jijini Dar es Salaam
ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani wateja 400
wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.
Tawi hilo limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa
ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Osysterbay na maeneo ya jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Kaim
Meneja wa CRDB, Godlisten Mtei alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo
ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo.
Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa
wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na
watu mbalimbali.
“Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki, na tunazidi kuwakaribisha
wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benko yetu na pia
tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka fedha
(ATM) ambayo hufanyakazi masaa 24”alisema.
Mtei alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na TemboCardVisa, Akaunti ya
Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account pamoja, Malikia
akaunti ambayo ni maalum kwa wanawake na Akaunti ya Akiba.
Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya
Tanzanite, huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima ili kuzidi
kuwapatia huduma bora wateja wao.
Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa likitoa huduma ya
kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking), pamoja na Akaunti ya
Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account.
Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya kutumia tawi hilo pekee
katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali
mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali.
Katika hatua nyingine Meneja Mauzo wa benki hiyo Richard Joseph alisema,
katika harakati za kufanikisha wananchi wanajiunga na benki hiyo
wameamua kuweka tawi katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam ambapo
kwa siku zaidi ya watu 70 wanaojiunga na benki hiyo.
No comments:
Post a Comment