Ahadi Mwandeko (22) amenyofolewa nyama mkononi akiwa
usingizini.
|
MWALIMU wa Shule ya msingi Motomoto iliyoko katika kijiji
cha Motomoto kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali Mkoani hapa, Ahadi Mwandeko (22)
amenyofolewa nyama mkononi akiwa usingizini.
Mwalimu huyo ambaye alikutwa na jeraha katika mkono wake
wa kulia asubuhi baada ya kutoka kuamka alisema hajia ni kitu gani kilichomzuru
hadi kufikia kuwa na jeraha kubwa mkononi.
Akizungumzia mkasa huo alipotembelewa na waandishi wa
habari shuleni kwake Mwalimu Mwandeko alisema akiwa usingizini aliota kama
anaugomvi na mwanamke ambaye hakuitambua sura yake, lakini baada ya kuamka
asubuhi alijikuta akiwa na jeraha huku likivuja damu
nyingi.
Alisema baada ya kukuta hali hiyo alienda kwa Mwalimu
mkuuwa shule hiyo Lyidia Mdowe kwa ajili ya kumpa taarifa ya jambo lililomkuta
ambapo alishauriwa kwenda Hospitali kwa ajili ya
matibabu.
Aliongeza kuwa baada ya kufika katika Zahanati ya Ruiwa
alipatiwa matibabu na kurejea shuleni ambapo Mwalimu mkuu alitoa taarifa kwenye
Serikali ya kijiji ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Kassim Mwagalla aliitisha
mkutano wa hadhara.
Mwalimu Mkuu Mdowe alisema hali hiyo imezua hofu kwa
walimu wengine ambao ni wageni kiasi kwamba hata ari ya ufundishaji imepungua
baada ya kuona yaliyotendeka kwa mwalimu mwenzao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Kassimu
Mwagalla ambaye alilihusisha tukio hilo na ushirikina alitoa rai kwa wanakijiji
kuacha vitendo hivyo kwa kuwa vinadhoofisha utendaji kazi wa watumishi hususani
walimu ambao si wazawa wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa tabia hiyo ikizidi kuendelea itasababisha
walimu kuondoka ili kukimbia kupatwa na matatizo kama hayo ambayo hayasaidii
maendeleo ya kijiji chao.
Pia aliwasihi kuacha mara moja tabia hiyo ambapo
aliongeza kuwa mtu yoyote atakayebainika kuhusika na sakata hilo atahamishwa
kijijini hapo ambapo pia aliwataka wakazi waliohamia eneo hilo kinyemela
kujiandikisha ili kijiji kiwatambue.
Baadhi ya wanakijiji waliozungumza na waandishi wa habari
walionekana kushangazwa na vitendo hivyo ambapo walisema dunia ya sasa ni
tofauti na zamani ambayo walikuwa wakiamini kwenye
ushirikina.
“ Mtu yeyote aliyekula nyama ya mwalimu huyu airudishe la
sivyo tukimuona nay eye atakiona cha moto lakini pia haya mambo yalipitwa na
wakati yalikuwa yakifanyika zamani bora wayaache” alisema Moses Njeje mkazi wa
kijiji cha Ruiwa.
Chifu wa eneo hilo Shadrick Melele alipotafutwa
kuzungumzia hali hilo amekemia vitendo hivyo ambapo pia amesema kuna mwanamke
ambaye anasadikiwa kuhusika na tukio hilo amejitokeza na kumwomba msaada
chifu.
Hata hivyo Chifu huyo aliahidi kulifanyia kazi sakata
hilo na kulitafutia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuwaonya wanaohusika na matatizo
hayo ambapo Kata hiyo imekuwa ikijihusisha na matukio mengi ya kishirikina
ambayo yamewahi kuripotiwa likiwemo la Chifu mwenyewe kunusurika kuzikwa akiwa
hai.
Na E.Kamanga Mbeya
No comments:
Post a Comment