Saturday, March 16, 2013

Askofu Kinyunyu Dodoma, amlilia tena Askofu Laizer


Aliyepiga magoti ni Askofu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayaosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu katika ibada ya kumweka wakfu kuwa askofu wa tatu wa Dayosisi hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.
Thomas Laizer wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati, Arusha
mjini hivi karibuni.

Na Bryceson Mathias, Dodoma.

ASKOFU Amoni Kinyunyu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi  ya Dodoma, amejikuta akimlilia tena Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Askofu Dk Thomas Olmorjor Laizer (69), baada ya kutoneshwa na Kifo cha aliyekuwa Mzee wa Kanisa na Mwenyekiti wa Fedha Dayosisi yake Lowasa Ole Sikoi wa KKKT Chinangali.

Kinyunyu altoa masikitiko hayo Jumatatu, Machi 11th, 2013 alipohubiri katika Ibada ya kuuaga mwili wa Sikoi Chingali KKKT tayarii kwa kuusafirisha kwenda nyumbani kwake Arusha, baada ya kufariki kwa Shinikizo la Damu Jumamosi, Machi 9th, 2013.

Akizungumzia pigo ambalo KKKT Dodoma imepata kwa kuagana na Marehemu Sikoi, Askofu Kinyunyu alifananisha na KKKT ilivyopata Pigo kwa kuagana na Askofu Laizer kutokana Jinsi Walivyolitumikia Kanisa kwa Mali zao, Muda, Akili na Chochote walichokuwa nacho pamoja na kuwasaidia wengine.

“Wakati nikiwa Mkuu wa Jimbo, nilimshuhudia Sikoi akilinisaidia Kanisa Dodoma kwa kila kitu alichokuwa nacho, ambapo hata nilipokuwa naona tumekwama Jambo fulani katika AMendeleo ya Kanisa Kirohona Kimwili, ukimuita Sikoi alitoa Ufumbuzi wake mara moja na Jambo likafanikiwa.

“Unapotaja KKKT Dayosisi ya Dodoma, usimtaja Sikoi utakuwa hujasema kitu, maana hata Kiwanja cha Kanisa hili tunapomuagia sasa, kilikuwa cha kwake lakini kwa moyo wa kulipenda Kanisa na Watu alikitoa kwa Kanisa ijengwe Nyumba ya Kuabudia.

Hata humo ndani wamo watu waliosaidiwa Kazi au Hali na Mali kama Kanisa lilivyosaidiwa na Sikoi na leo hii lina na Maendeleo kama mlivyo ninyi alivyowasaidia, hivyo msije Mkamsahau Mjane na Watoto wake! Kwa hiyo kumbukeni wema wake na sisi Kanisa tutafanya hivyo”.alisema Askofu Kinyunyu.

Msiba wa Sikoi ambao ulijaa Maelfu ya watu, uliwaacha watu wakilia na kuomboleza, hasa wakikumbuka Kazi alizolifanyia Kanisa zinazoonekana hadi leo kwa macho, ambapo ilifika mtu mgeni anapoelekezwa au kueleza mahali aliposali kama ni Chinangali KKKT, walizoea kusema Kanisa la Sikoi.

Aidha hadi anafariki, Sikoi alikuwa Kiongozi na Mjumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi Kuu ya KKKT Dayosisi ya Dodoma, ambayo kwa miaka 22 sasa ilikuwa haina Ofisi ya Dayosisi inayolinganishwa na Ukubwa na wingi wa Waumini nchini na mkoani hapo.

No comments:

Post a Comment