Bango Maalum Kwa ajili ya Kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa (NEPAD) Alipo fanya Ziara yake leo katika Mamlaka ya Chakul;a na Dawa (TFDA) |
Mamlaka ya chakula na Dawa
TFDA imetembelewa na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi iliyopo chini ya Umoja wa Africa New Partnership for Africa’s
Development Agency (NEPAD) Dr, Ibrahim Assane Mayaki ambapo
amesema kuwa amefurahishwa na Utendaji kazi wa TFDA katika Udhibiti wa
Chakula na Dawa.
Dr Mayaki ameisisitiza TFDA kuwa na ushirikiano wa
pamoja Africa nzima ili wawe na mtazamo unaofanana ili kuweza kuboresha Bidhaa
zote za Afrika kwa ujumla katika Kiwango cha Kimataifa.
“Tunataka Africa iwe
na Mtazamo unaofanana ili kama bidhaa ikliwa haina kiwango cha ubora basi bidhaa hiyo ikataliwe Africa
nzima,” amesema Dr Mayaki.
Aidha Dr Mayaki ameonyesha
kufurahishwa na Maabara ya TFDA ambapo amesema kuwa ni Maabara yenye kiwango
kinacho kubalika kimataifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFDA akimkabidhi Zawadi maalum Dr, Mayaki kama ishara ya Kumpongeza kwa kufanya Ziara yake TFDA |
Mayaki yupo Makini kuongea na waandishi wa habari |
Wafanyakazi wa TFDA wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Dr Mayaki |
No comments:
Post a Comment