Balozi wa
Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram Mukama Biswalo (kulia)
akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto),
baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Adis
Ababa, akitua kwa muda kwenye Uwanja huo akiwa safarini kwenda China kwa
ziara ya kikazi. Wengine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Zanzibar), Vuai Ali Vuai na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk.
Asha-Rose Migiro na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Titus Kamani.
Msaidizi wa
Katibu Mkuu wa CCM, Edward Mpogolo (kushoto) na Ofisa anayeshughulikia
Siasa za Kimataifa, Makao Makuu ya CCM, Amos Siantemi wakiratibu
taratibu za safari ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
kwenda China, leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Maofisa hao pia walikuwa sehemu ya msafara huo.
Mkuu wa
Kitengo cha Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa wa Makao Makuu ya CCM, D.
U. H. Mshana na Mkuu wa Kitengo cha Sera za Jamii na Mahusiano ya Umma,
Jasinta Mboneko na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa ya CCM, Juliana Chitinka wauaga ujumbe wa CCM wakati ukiondoka
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliokuwa ukienda china
kwenye ziara ya kikazi ya siku kumi ikiongozwa na Kinana.
Baadhi ya
viongozi na maofisa wa Chama waliopo kwenye msafara huo wakiwa kwenye
basi maalum kwenda kupanda ndege ya Ehiopian Airlines wakati wa safari
hiyo,
Baadhi ya
viuongozi na maofisa wa Chama wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Addis
Ababa baada ya msafara wa Kinana kutua kwa saa sita kwa ajili ya
kuendelea na safari ya kwenda China jioni hii. (Picha zote na Bashir
Nkoromo)
No comments:
Post a Comment