Muungano wa CORD
wake Raila Odinga umeelezea kuwa unajianda kwenda mahakamani kupinga
matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.
Raila Odinga, amewaambia waandishi wa habari kuwa matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalikuwa yamehujumiwa hasa baada
ya kutokea hitilafu katika mitambo ya elektroniki iliyokuwa inatumiwa
katika shughuli hiyo.
Raila amedokeza kuwa muungano wao unajiandaa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Aidha alisema kugoma kwa mitambo hiyo
kulichanganya mambo katika shughuli ya kuhesabu kura. Alisema kuwa baada
ya kutokea hitilafu, kura alizokuwa amepata katika maeneo bunge ambayo
ni ngome zake , ziliongezwa kwa hesabu ya kura za muungano pinzani wa
Jubilee.
Mapema wiki hii, wakati shughuli ya kuhesabu
kura za urais ilikuwa inafanyika, CORD walielezea malalamishi kuhusu
shughuli nzima hasa baada ya kura kuanza kuhesabiwa kwa mikono badala ya
mashine.
Lakini mahakama kuu ilitupilia mbali kesi yao
ikisema kuwa haina uwezo wa kufanya uamuzi katika kesi hiyo, na kuwa ni
mahakama ya juu zaidi pakee inayoweza kusikiliza kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment