Friday, March 8, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL YA INDIA BW SUNIL MITTAL IKULU, DAR ES SALAAM

 Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Airtel pamoja na Waziri wa Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa (kushoto). PICHA NA IKULU
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Sam Elangallor.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal na ujumbe wake alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Airtel na wa Serikali jana jioni Ikulu Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Mkurugeni Mkuu mpya wa Airtel Tanzania Bw Sunil Colaso na aliyemaliza muda wake Bw Sam Elangallor (kulia).
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Airtel India Bw. Sunil Mittal alipokutana naye Ikulu, Dar es salaam, jana jioni.

Na Mwandishi Maalum

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana jioni amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bharti Airtel ya India Bw. Sunil Mittal aliyemtembelea na ujumbe wake kuzungumzia maswala mbalimbali ya sekta ya Mawasiliano. Bw. Mittal aliongozana na Bw. Manoj Kohli, CEO Internationa wa kampuni hiyo, Bw. Jayant Khosla, CEO Anglophone Africa, Bw. Sam Elangallor, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania anayemaliza muda wake, Bw Sunil Colaso, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Airtel Tanzania pamoja na Bi Beatrice Singano, Corporate Affairs Director  wa Airtel Tanzania.


Katika mazungumzo hayo ujumbe wa serikali ulikuwa ni pamoja na Waziri wa Sanyasi, Mawasiliano na Tekenolojia, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CHC Profesa Marcelina Chijoriga, Kaimu Mtendaji wa CHC Bw. Dome Malosha, Msajili wa Hazina Mama Mlaki na Mhandisi Clarence Isokeleza

No comments:

Post a Comment