Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kuzindua rasmi taarifa ya
utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti
wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua
juu baada ya taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria
mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda', Kushoto kwake ni
Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia
baada ya kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na
malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es salaam.
Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt
William Mgimwa.
Wadau kutoka sekta mbalimbali
wakiangalia matangazo ya kupiga vita UKIMWI na Malaria wakati wa
uzinduzi rasmi wa taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria
mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam.
Meza kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi
(TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya
ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH) KIJITONYAMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia moja ya chupa ya dawa ya kuongeza virutubisho mwilini,
Juice Lishe,(Morizella
Juice) huku akimsikiliza Dkt. Modest Kapingu, kuhusu matumizi ya dawa
hiyo, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya
Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013
kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala
ya kisayansi. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimsikiliza MMtafiti wa TEHAMA kutoka COSTECH, Rahma Bashary, wakati Makamu
alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo
ya tume hiyo
inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kulia ni, Waziri
wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai, Dkt. Flora Tibazarwa,
wakati Makamu
alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27, 2013 kujionea maendeleo
ya tume hiyo
inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa
Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa namna ya kutumia simu ya mkononi kuunganisha huduma ya mtumiaji
simu ili kupata taarifa ya mkulima kutoka kwa Gwaliwa Mashaka wa
Kampuni ya Spendid Amos, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea
katika maonyesho
ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo Machi 27,
2013 kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa
masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Kisayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia, leo Machi 27, 2013.Picha na OMR
DOUBLETREE BY HILTON YAKABIDHI TAA ZA KUTUMIA MIONZI YA JUA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MIKOCHENI A
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam, Salehe
Makwiro (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa taa 200 za kutumia mionzi
ya jua kwa ajili ya wananfunzi wa darasa la saba ambao watazitumia kwa
ajili ya kujisomea. Kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Doubletree
by Hilton, Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa Doubletree by Hilton,
Sven Lippinghof.
Meneja Mkuu wa Doubletree by Hilton, Sven Lippinghof akiwaelekeza
wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam jinsi ya
kutumia taa zinazotumia mionzi ya juu mara baada ya kukabidhi taa 200
kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya
Doubletree by Hilton, Florenso Kirambata akiwafundisha jinsi ya kutumia
taa zinazotumia mionzi ya jua wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A
jijini Dar es Salaam leo, wakati uongozi wa hoteli yhiyo ulipokabidhi
msaada wa taa 200 kwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo kwa
ajili ya kuwasaidia wakati wa kusoma. (Picha na Habari Mseto Blog)
ADVANC BANK WAZINDUA TAWI JIPYA TEMEKE DAR
Mwakilishi wa Mbunge wa Temeke, Thabit Mussa akikata utepe wakati wa
uzinduzi wa jengo la benki ya Advanc, Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Peter Moelders na kulia ni Kaimu Meneja
wa benki hiyo, Boniface Mhali na diwani wa Temeke, Hamisi Msombo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Advanc, Peter Moelders akisakata muziki wa asili na msanii wa kundi la
Wanne Star, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, Temeke jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la Wanne Star na
kundi lake akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki mpya ya Advanc,
Temeke jijini Dar es Salam jana
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya Advanc imetakiwa kuonyesha tofauti
yao na benki zingine kwa kutoa riba nafuu na masharti yanayowezekana kwa
wakopaji ili kulisaidia Taifa kiuchumi kupitia wajasiriamali wadogo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo
wilayani Temeke jana, mwakilishi wa mbunge wa Temeke, Thabit Massa alisema
ingawa kuna benki nyingi nchini lakini riba na masharti magumu yanafisha ari ya
watu kukopa.
Mwakilishi huyo wa mbunge alisema kufunguliwa kwa tawi hilo
kunafanya Temeke kuwa na matawi saba sasa ya benki lakini bado hakujawa na
mafanikio tarajiwa na mbaya zaidi baadhi ya benki hizo hazina huduma nzuri kwa
wateja.
“Lugha nzuri hakuna na hata mikopo imekuwa ikitolewa kwa
kujuana baina ya wakopaji na watendaji wa baadhi ya benki jambo ambalo sio jema
na linashusha imani ya wateja kwa benki” alisema na kuongeza kuwa anatarajia
mabadiliko.
Alisema beni hiyo inatakiwa ije na mambo tofauti ili kuleta
tija kwa wakazi wa eneo hilo tofauti na ilivyo sasa na awali Mtendaji mkuu wa
benki hiyo, Moelders alisema wamekuja ulata mapinduzi makubwa katika uduma
za kibenki nchini.
“Benki yetu walengwa wake na wananchi wa kawaida na wale
waliopo vijijini na kabla ya mwisho wa mwaka huu itafungua matawi mawili Jijini
Mwanza na mwakani watazindua matawi mengine ya idadi hiyo Jiji la Mbeya.
Alisema
SIRI YA KUUAWA KWA ZITTO KABWE
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ Dk. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza’.
Habari
hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga
kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa.
Napenda kusema yafuatayo:
Moja,
sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane
na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu
kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio
tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi
kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela
Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba
mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili,
Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua
maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi
ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa
kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu.
Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama
kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake
atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo,
fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha
niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni
kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia
ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
Tatu,
nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie
muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya
chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA
anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa
anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina
langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la
watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa
anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye
vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda
kama ni malengo ya taasisi.
Nne,
Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu
kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk
kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu
demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama
chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013
UJUMBE WA FIFA KUSIKILIZA WAGOMBEA TFF APRILI 16
SHIRIKISHO
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na
baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake
nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe
huo ambao moja ya shughuli zake kuwasikiliza wote walioenguliwa na
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na hawakuridhika na uamuzi huo,
utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais
wa TFF, Leodegar Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na
kutoa ripoti kwa mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa
mwongozo.
Ujumbe
huo utakutana na pande mbalimbali zinazohusika wakiwemo wagombea,
kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia ujumbe huo unatarajia kumtembelea
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi
wa viongozi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini
ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa
kulalamika kuwa hawakutendewa haki na wangependa shirikisho hilo
liingilie kati.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
HISPANIA YAIZABUA UFARANSA NYUMBANI STADE de FRANCE
Paul Pogba wa Ufaransa, akimrukia na kumshika kiungo wa Hispania, Xabi
Alonso, tukio ambalo lilimfanya aoneshwe kadi ya pili ya njano na
kupigwa 'red-card' iliyomtoa nje ya uwanja kunako dakika ya 78 ya
pambano la kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lililoisha kwa Hispania
kuwachapa wenyeji Ufaransa bao 1-0 kwenye dimba la Stade de France
jijini Paris usiku wa kuamkia leo.
Kiungo Xavi Hernandez wa Hispania akionywa kwa kadi ya njano na mwamuzi
Viktor Kassai wa Hungary katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia
2014 kati ya Ufaransa na Hispania.
Paul Pogba wa Ufaransa (wa pili kulia
mwenye jezi namba 19), akioneshwa 'red-card' iliyomtoa nje ya uwanja
katika dakika ya 78 ya pambano la kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014,
lililoisha kwa Hispania kuwachapa wenyeji Ufaransa bao 1-0 kwenye dimba
la Stade de France jijini Paris usiku wa kuamkia leo.
Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema (katikati) akitafuta mbinu za
kuwatoka wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania katika mechi baina ya
nchi hizo jana usiku.
Mlinda mlango wa Ufaransa, Hugo
Lloris (kushoto) akijaribu kuokoa mpira wa Pedro usitinge katika nyavu
zake. Jitihada ambazo hazikuzaa matunda, hivyo mpira kutinga nyavuni
kuandika bao pekee la Hispania.
Kipa Hugo
Lloris akiukodolea macho mpira uliopigwa na Pedro ukitinga nyavuni
kuiandikia Hispania bao pekee katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la
Dunia 2014.
Pedro akishangilia bao hilo.
Hii ilikuwa ni mapema kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu, Paul Pogba
akichuana na viungo bora na mahiri duniani wa timu ya taifa ya Hispania,
Xavi na Andres Iniesta.
Kipa wa Hispania, Victor Valdes, akijiandaa kuzuia shuti la winga wa
Ufaransa, Frank Ribery, huku beki Gerrard Pique akiwa tayari kumsaidia.
Beki wa kushoto wa Ufaransa, Patrice Evra (kulia) akizuia shuti jepesi la mshambuliaji David Villa wa Hispania.
No comments:
Post a Comment