Mashabiki
wa Bar ya East Africa wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi
wakati wa shindano la Safari Nyama Choma lililofanyika katika Viwanja
vya CCM Mkoa Mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi (wa pili kulia) akimkabidhi
kitita cha sh. milioni moja Meneja wa Bar ya East Africa,Godfrey Mawala
(kulia), baada yakuibuka washindi wa kwanza katika shindano la Safari
Lager Nyama Choma lililofanyika Moshi Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo.Wapili kulia ni Mpishi Mkuu Wilfred William na
Meneja Mauzo wa Moshi, Edmundi Rutaraka
Na Mwandishi Wetu, Moshi
EAST
AFRICA BAR, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa
Moshi, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano
hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Safari Lager.
Kwa
kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye
Viwanja vya CCM Mkoa , baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja
pamoja na cheti.
Waliokuwa
mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani hapa, Makanyaga Bar,
walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti,
wakati White Star Pub walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh
600,000 na cheti.
Walioibuka
na nafasi ya nne ni baa ya Forest Bar iliyozawadiwa Sh 400,000 na
cheti, wakati baa ya Lamina ilishika nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh
200,000 na cheti.
Akizungumza
kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu,
alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa
kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja
vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na
mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa
vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager
kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani ambao ndio mkoa wa mwisho.
“Tulianza
kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika
shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Moshi tukapata baa hizi tano
zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua
watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema
tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,”
alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo ndio inayoongoza kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi,
aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema
kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa
Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari
Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali
kama soka na mingineyo.
“Mashindano
haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na
salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.
Alizitaka
baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga
kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment