Mafundi Wakipongezana: Viungo mahiri wa
FC Barcelona ya Hispania, Andres Iniesta (kushoto) na Xavi Hernandez
wakipongezana baada ya Barca kupata bao la kusawazisha dhidi ya PSG ya
Ufaransa, lililowawezesha kutinga nusu fainali ya Mabingwa Ulaya.
Nafunga Kama Ifuatavyo: Javier Pastore
wa PSG (kulia), akipiga shuti kufunga bao la kuongoza katika mechi ya
marudiano robo fainali mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona, kwenye Uwanja
wa Nou Camp na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, matokeo yaliyoipa Barca
tiketi ya kucheza nusu fainali.
Kitu Kambani Kudadadeki: Mlinda mlango
wa Barca, Victor Valdez (kulia) akishuhudia mpira ukitinga nyavuni
kuiandikia PSG bao la uongozi lililofungwa na Pastore (wa pili kushoto),
huku beki Dani Alvez akiwa chini.
Umetishajeeeeee!! Pastore (kushoto) akishangilia bao hilo pamoja na Ezequiel Lavezzi na Zlatan Ibrahimovich.
Maji Yalipozidi Unga: Baada ya kukosa
mbinu za kuipenya safu ya ulinzi ya PSG, Barca ikafanya 'sub ya ukweli.'
Hapa Cesc Fabregas akitoka kumpisha Lionel Messi aliyekuja kuibadili
timu.
Kafanye Mambo Mtu Wangu!! Fabregas akimshika kichwa Messi huku akimpisha kuingia dimbani kufanya mambo muhimu kwa timu.
Pande la Bao Muhimu: Faida ya
mabadiliko yaliyomtia Messi dimbani ikaanzia hapa. Mshambuliaji Pedro
Rodriguez wa Barca (17), akipiga shuti kuifungia timu yake bao, baada ya
kupokea pande la mwisho kutoka kwa mtokea benchi na majeruhi, Messi.
Kimeelewekaaaaa!!!! Pedro akishangilia bao lake.
Furaha ya Bao: Wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi Barca, wakishangilia bao la Pedro
We Can't Believe!!! Wachezaji wa PSG,
Ibrahimovich na Pastore wakishika viuno vyao wakati wa kuanziasha mpira
baada ya kufungwa bao na Barca.
Hatuna Chetu Hapa!!! David Beckham
(katikati), akiondoka uwanjani na nyota mwenzake wa PSG, baada ya
filimbi ya mwisho ya mchezo.
Tumefuzuuuuuuu!!!! Wachezaji na maofisa
wa benchi la ufundi Barcelona, wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho
na kujihakikishia tiketi ya kucheza nusu fainali.
Jijini Turin Nako Mambo yalikuwa Hivi:
Kiungo Fundi, Andrea Pirlo wa Juventus Turin ya Italia, akipiga 'free
kick' wakati wa mechi yao ya marudiano dhidi ya Bayern Munich ya
Ujerumani, iliyoisha kwa Bayern kushinda 2-0 na kufuzu nusu fainali kwa
ushindi wa jumla wa mabao 4-0.
Huniwezi Dogo: Kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Ruben akimtoka beki wa Juventus katika mechi hiyo.
Nakutoka Kama Hivi:Nyota wa Juventus Turin, akimtoka kiungo wa Bayern, Bastian Schweinsteiger wakati wa mechi hiyo.
Mshambuliaji wa Bayern, Mario Mandzukic (9), akiifungia Bayern bao moja kati ya mawili yaliyoipa ushindi dhidi ya Juventus.
Mandzukic akishangilia bao hilo.
Daka na Hiyo!!! Mtokea Benchi Claudio Pizarro wa Bayern, akipiga shuti kuifungia timu yake bao dhidi ya Juventus.
Raha ya Mechi Bao: Pizarro akishangilia bao hilo.
Superfans: Mashabiki wa Bayern, wakishangilia timu yao ilipokuwa ikiizabua Juventus.
No comments:
Post a Comment