Rais wa Chama sha Walimu Tanzania CWT akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika makao akuu ya Chama hicho. |
Chama Cha Walimu
Tanzania (CWT) kimewataka walimu wote Tanzania, Bunge la Tanzania pamoja
na wazazi wa Wanafunzi kuungana kwa
pamoja, kuilazimisha Serikali kukubali
kukaa meza moja na CWT kujadili
mishahara pamoa na Posho za Walimu kwa ajili ya Mwaka ujao wa Fedha.
Rais wa CWT Bw, Gratian Mukoba, ameyasema hayo leo katika
mkutano wake na waandishi wa habari
uliofanyika katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salam.
Bw , Mukoba amesema kuwa chama kimefikia uamuzi huo wa
kuwashirikisha walimu wote pamoja na wazazi na Bunge baada ya Serikali kukataa
kurudi mezani kujadiliana na CWT Kuhusu mishahara na posho za walimu wa Mwaka wa Fedha
wa 2013/2014.
Amesema kuwa, baada ya Mahakama kuamuru CWT kurudi Mezani
kwenye hukumu ya tarehe 02 Agosti 2012,
CWT iliandika barua kuieleza serikali
kuwa chama kipo tayari kukutana kwa
ajili ya Majadiliano, lakini Mh Philip
Mulugo Naibu waziri wa Elimu aliagiza hoja za kujadiliwa katika kikao hicho kuwa ni hoja zilizo
sababisha walimu kugoma, jambo ambalo CWT kilipinga, kwa maelezo kuwa Serikali
haikuwa na nia thabitiya kujadiliana na CWT.
“Serikali na CWT, ilikutana tarehe 09 januari 2013 kwenye Baraza a Majadiliano na
walimu ambapo CWT Kilikubaliana na hoja
ya Serikali kufanya Majadiliano japokuwa CWT, Tangu mwanzo hakikuona nia thabiti
ya serikali kujadilana ambapo CWT kilitakiwa kuandaa hoja yake ya kuwasilisha
kabla ya majadiliano kuanza,ambapo chama kiiwasilisha lakini Serikali
ilishindwa kutoa Majibu”, amesema Mukoba.
Ameongeza kuwa Serikali iliweka msimamo wake wa kutokujadili
mishahara ya walimu baada ya Makatibu
wakuu wa TALGWU, TUGHE, CWT, na TUCTA kukutana na Katibu mkuu kiongozi Ikulu
jijini Dar es Salaa, katika kikao cha Tarehe 02 Aprili, 2013 kilichohudhuriwa
na Makatibu wakuu wa Utumishi, TAMISEMI.
Aidha CWT kimetaka wito huo kuzingatiwa kuhakikisha kuwa
Maslahi ya walimu, yanapatikana ili kuepusha Mgogoro unaoweza kujitokeza ikiwa
Serikali itaamua kujipangia Mishahara ya Walimu bila kujadiliana na CWT.
Nasisitiza Jamani tuungane Walimu na wazazi kutetea Maslahi ya walimu kuepusha mgogoro utakaosababisha wanafunzi milioni 10 kukosa masomo ikiwa walimu watagoma. |
No comments:
Post a Comment