Friday, April 5, 2013

NMB YAWAPA SEMINA WAJASIRIAMALI JIJINI DAR

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kulia), akizungumza wakati mkutano na wanachama wa NMB Business Club, Kanda ya Temeke, uliofanyika leo, Mbagala, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ezekiel Gutti, Meneja wa Mikopo Midogo Midogo ya Biashara wa benki hiyo, Mashaga Changarawe na Loelia Kibassa ambaye ni Meneja wa Mikopo ya Kati ya Biashara. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Mwanachama wa NMB Business Club Kanda ya Temeke, Hermetus Urassa akichangia mada wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NMB Business Club Kanda ya Temeke, Ezekiel Gutti akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanachama wa club hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Mikopo Midogo Midogo ya Biashara wa benki hiyo, Mashaga Changarawe na Meneja wa Mikopo ya Kati ya Biashara,  Loelia Kibassa.
 Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika warsha hiyo.
 Mmoja wa wajasiriamali akichangia mada.
 Meneja wa NMB tawi la Temeke, Halord Lambileki akiwa maofisa wa NMB. 

DAR ES SALAAM, Tanzania


WAFANYABIASHARA wa Kati wa Wilaya Temeke wamesema kuwa kuendelea kwao kiuchumi kunahitaji ubunifu pamoja na uaminifu katika mikopo wanayopata katika taasisi za fedha.

Hayo waliyasema na wafanyabiashara hao walipokutana katika Mkutano uliondaliwa na Benki ya NMB wakati wa mafunzo ya uendeshaji wa biashara kupitia huduma ya mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo uliofanyika leo katika viwanja vya Dar Live Jijini Dar es Salaam.

Mfanyabiashara wa Vifaa vya Maofisini, Hellen Mchopa alisema kuwa amejifunza mengi katika mkutano na kufungua ukurasa mpya wa kufanya biashara nyingine kutokana na mtaji aliofikia pamoja na kuwa na uhakika wa kupata mikopo katika benki ya NMB.

Alisema kuwa benki ya NMB imemuokoa kuondokana na umasikini kwa kumjengea uwezo kuwa mchumi katika fedha ambayo anaendeshea biashara yake inayotokana na benki hiyo.

Hellen alisema kuwakutanisha wafanyabiashara ambao ni wateja wa NMB wanapata fursa ya kujifunza pamoja na kutanua biashara zao  kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.
  
Mfanyabiashara wa Duka la Vyakula vya jumla Baraka  Nicolous alisema kuwa kupitia mkutano kumemuondoa katika kuwa na biashara moja ambapo kutokana fursa hiyo anaweza kuanzisha biashara nyingine kwa kupata mawazi kwa wafanyabiashara ambao wanazifanya na kuwaletea tija ya mafanikio.

Nicolous alisema kuwa mtaji alianza na milioni 1 mwaka 2002 ambapo sasa amefikia mataji wa milioni 15 ambapo anaweza kukopa zaidi ya sh.milioni 15 kutoka katika benki ya NMB.

Mafanikio yetu yametokana na benki ya NMB kuwa na huduma ya mikopo kwa wajasiriamali ambapo tumeweza kusomesha watoto kufanya ujenzi wa nyumba huku biashara zikiendelea.

No comments:

Post a Comment