Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Eng, Zebadia Moshi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Matokeo ya Usajili Mpya wa Vyuo vya Ufundi Stadi. |
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya VETA Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Eng Zebadia Moshi amesema kuwa, Mabadiliko hayo yamesababisha, Mamlaka kufanya Mapitio tena ya Vigezo vinavyotumika katika kusajili vyuo vya vya Ufundi Stadi ili viweze kuandaa wanafunzi Mahiri watakao weza kuhimili Ushindani unaoletwa na Mabadiliko tajwa.
Eng Moshi, Ametaja Sifa Mpya za Kusajilili Chuo ni kama Ifuatavyo:
- Uongozi Bora vwa Chuo
- Vifaa vya Kufundishia Vya kutosha kulingana na Mitaala
- Majengo ya Kufundishia ya Kutosha na yenye Viwango vinavyotakiwa
- Uwezo wa kifedha wa chuo ikiwa ni pamoja na Utunzaji.
Aidha Eng Moshi amevitaka vyuo kuweka cheti cha Usajili wake katika Notice board ya Chuo na kuandika namba ya Usajili kwenye bango linaloonyesha chuo kilipo.
"Kwakuweka namba ya Usajili kwenye Notice board tutatambua vyuo visivyo vya VETA kwa namba ya Usajili," amesema Moshi.
No comments:
Post a Comment