Tuesday, April 16, 2013

WABUNGE WATOANA MAPOVU BUNGENI.....NENO "IMPOTENCY" LAWAFANYA WATOFAUTIANE


Ilikuwa  ni wakati wa kuchagia hotuba ya Waziri mkuu ambapo Mheshimiwa Wenje (CHADEMA) aliichamba  serikali na kuonyesha kwamba haina uwezo wa kutatua matatizo.

Ikafika mahala mheshimiwa Wenje akatumia sentensi mbili za kiingereza na akatamka kwamba it shows that the gorvement is IMPOTENT.


Binafsi sina matatizo na English, neno
IMPOTENT na deritaives zake nalifahamu maana zake nyingi, na katika public maana yake kubwa ni hiyo aliyotumia Mh. Wenje.

Niliendelea kusikiliza bunge nikijua kwamba wabunge wetu nao hawana tatizo na kiingereza na sikutarajia lolote na matumizi ya neno hili kama ambavyo siwezi kutegemea matatizo Julius Nyerere alipomwambia Augustine Mrema kwamba {
I cant go to sleep in Butiama and let my country go to dogs}

Wakati ule Nyerere alimjibu Mrema kuwa aache kampeni zake za urais kwani yeye kama Nyerere atampigia kampeni Benjamin Mkapa.


Mrema aliibuka na kutangaza kwamba Nyerere kawatukana wapinzani kuwa ni mbwa.


Leo, wabunge wa CCM wakanikumbusha kituko hiki cha Mrema kwa wao kusema kwamba Mh. Wenje afute kauli yake kwani IMPOTENT maana yake ni kuwa Hanisi yaani kutokuwa na uwezo wa kutozaa.


Mwanzoni nilidhani ni mmoja tu, bwana, wameibuka wawili wakidai afute kwa maana hiyohiyo na wengine wana CCM wakishangilia hata waliokuwa mawaziri ambao wanasafiri kila siku kwenda Uingereza na Marekani kunakozungumzwa kiingereza.


Je, neno
IMPOTENT lina maana hiyo kweli? Nimefungua dictionary yangu, {Oxford Advanced Learner's Dictionary, Seventh Edition, ISBN: 9780194316613, pg.749}inasema hivi: 1: Having no power to change things or to influence a situation. E.g. POWERLESS {Without the chairmans support the commitee is impotent}, {She blazed with impotent rage}.
2: (of a man): unable to achieve an erection and therefore unable to have full sex


Na hata online dictionary mnaweza kusoma wenyewe kwenye link hii (Click
Here)
Neno
IMPOTENT linatokana na neno la kitalini yaani POTENT literacy meaning "being powerful". Ndiyo maana unaposema Afrika ina mali POTENTIAL maana yake nguvu ya mali iliyojificha.

TUnaposema mlima una potential volcano maana yake ni volcano yenge nguvu iliyofichika. Wakatoliki husema kanuni yaani Imani kwa kilatini wakisema {Credo in unum Deum, Patri
OMNIPOTENTE}. Maana yake Nasadiki kwa Mungu mmoja, baba mwenye nguvu zilizoenea pote. Hapa neno OMNIPOTENTE maana yake ni Mungu aliyeenea kote.

Kama wabunge  hawajui asili na maana ya neno POTENT na kama nao walipita shule za kata hawajui
POTENTIAL VOLCANO wakadhani ni volkano yenye matusi, basi ile tume ya kuchunguza kufeli kwa form four ipite na kwao pia.
By Nikupataje-JF

No comments:

Post a Comment