Mtu
mmoja aliyetambulika kwa jina la Swila William akiokolewa na Askari
katikati ya kundi la wana CCM baada ya kunusurika kupata kichapo na
wanaccm kwa kosa la kuingia katika mkutano wa CCM kisirisiri wakati yeye
ni Mtu wa CHADEMA.
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwanachama wa CHADEMA ameijikuta katika
wakati mgumu baada ya kuambulia kichapo kutoka kwa wanachama wa CCM
baada ya kujipenyeza katika mkutano wao wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi
ya Wilaya.
Mtu huyo alijefahamika kwa
jina la Swila William, mkazi wa Kalobe (50), na ambaye ni Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Sekondari Mshewe, amekubwa na masaibu hayo baada ya kuingia
katika mkutano kwa kitambulisho cha ‘Usalama wa Taifa’ bila kujua kuwa
anatambulika na baadhi ya WanaCCM. |
No comments:
Post a Comment