![]() |
Jocelyne
Maro Mii East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara
baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa
kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa
Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza
kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye
tmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota
Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima
ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi
wake.
|
(PICHA NA KAMANDA WA FULLSHANGWEBLOG)








![]() |
Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni. |








No comments:
Post a Comment